IQNA

Hizbullah yasisitiza kuwa haitajisalimisha

19:07 - July 05, 2025
Habari ID: 3480902
IQNA – Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Naim Qassem, amekataa wazo la kusalimisha au kuachana na silaha za harakati hiyo ya mapambano, akisema kuwa wanaotaka hilo wanapaswa kwanza kulaani na kutaka mwisho wa uvamizi wa Israeli dhidi ya Lebanon.

Akizungumza katika hotuba ya moja kwa moja kupitia kituo cha televisheni cha Al-Manar siku ya Ijumaa jioni, Sheikh Qassem alisema: "Wanaoitaka Hizbullah iache silaha zake, waambie kwanza hatari ya uvamizi inapaswa kuondoka. Haiingii akilini kuacha kukemea uvamizi halafu tuwatake wanaoupinga wainamishe vichwa na kujisalimisha."

Sheikh Qassem aliendelea kwa kusema: "Anayekubali kujisalimisha, lazima abebe mzigo wa uamuzi wake. Lakini sisi hatutakubali kamwe."

Alisisitiza kwamba: "Kulinda taifa si jambo linalohitaji ruhusa ya mtu yeyote. Ikiwa kutatolewa mbadala wenye uwezo wa kweli wa kulinda taifa, tupo tayari kujadili kwa kina takwa hio."

Matamshi haya yametolewa wakati ambapo Marekani, utawala wa Israel na washirika wao wamekuwa wakiishinikiza harakati ya Hizbullah kuacha njia ya silaha. Hata hivyo, harakati hiyo imefanikiwa mara kadhaa kulinda ardhi ya Lebanon dhidi ya mashambulizi ya kikatili yanayoongozwa na utawala wa Israel.

Katika tukio la hivi karibuni, Hizbullah iliweza kulazimisha utawala huo kukubali kusitisha mashambulizi baada ya mwaka mzima wa uvamizi na uhalifu dhidi ya watu wa Lebanon, kufuatia mashambulizi ya Hizbullah ambayo yalitekelezwa kuunga mkono kwa Wapalestina dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.

Hotuba ya Sheikh Qassem ilitolewa katika muktadha wa mwezi mtukufu wa Muharram, kipindi ambacho Waislamu duniani kote huadhimisha kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa Imam Hussein (AS), Imamu wa tatu wa Kishia. Sheikh Qassem alisisitiza umuhimu wa kutetea haki kama alivyofanya Imam Hussein dhidi ya ukandamizaji wa Yazid ibn Muawiya kala ya kuuawa shahidi katika mwaka wa 61 Hijria.

"Imam Hussein (AS) alifaulu. Huo ndio ushindi wa kweli," alisema Sheikh Qassem, akitambua urithi wa Imam Hussein miongoni mwa Waislamu ambao ni kusimama kidete kulinda ukweli bila kuyumba.

3493716

Habari zinazohusiana
captcha