IQNA

Haram ya Imam Hussein (AS) imeandaa tukio la Tuwairaj siku ya Ashura

18:29 - July 05, 2025
Habari ID: 3480899
IQNA – Wasimamizi wa Haram ya Imam Hussein (AS) huko Karbala, Iraq wametangaza kukamilika kwa maandalizi katika milango yote ya kuingilia kaburi hilo takatifu  kwa ajili ya kuwapokea waumini wanaoshiriki katika tukio la kuomboleza linalojulikana kama Tuwairaj.

Abdul Hassan Mohammed, afisa wa matengenezo, amesema ukarabati wa milango yote ya kuingilia umekamilika ili kupokea maelfu ya waombolezaji na waumini watakaoshiriki katika mbio za Rakdha Tuwairaj mnamo tarehe 10 ya Muharram (Ashura).

Aliongeza kuwa jitihada hizi zimetekelezwa chini ya mwongozo wa Sheikh Abdul Mahdi al-Karbalai, mwakilishi wa Ayatullah Ali al-Sistani.

Mbio za Rakdha Tuwairaj hufanyika kila mwaka huko Karbala siku ya Ashura. Katika tukio hilo, wafanyaziara hukimbia takriban kilomita 2–3 kuelekea Haram ya Imam Hussein (AS), ikiwa ni ishara ya mbio ambazo binamu wa mama wa Hadhrat Abbas (AS) walikimbia kutoka kijiji cha Tuwairaj (leo kinajulikana kama Al-Hindiya) hadi Karbala baada ya Vita vya Karbala mwaka 61 Hijria.

/3493719

 

captcha