IQNA

Maonyesho ya 'Qur'ani na Ashura' yafanyike eneo la Kashmir

15:37 - August 22, 2025
Habari ID: 3481118
IQNA-Maonyesho ya sanaa za Qur’ani na kidini yenye kichwa “Sanaa ya Mapenzi, Imani na Ashura” yalifanyika katika Chuo Kikuu cha Kashmir yakiratibiwa na Taasisi ya Utafiti wa Qur’ani ya Tebyan. Zaidi ya kazi mia moja za uchoraji, kaligrafia, picha na sanaa za kidigitali ziliwasilisha mada za Qur’an, Karbala na kujitolea.

Maonyesho haya yalivutia wanafunzi, walimu, wasanii na wapenzi wa sanaa, yakionyesha namna imani inavyoweza kuungana na ubunifu. Msanii mashuhuri Arshid Sauleh alieleza mbinu yake ya kuchanganya aya za Qur’an na mandhari za kisasa, akisisitiza kuwa Imam Hussein (AS) ni dhihirisho la Qur’an na kutojitenga na Ahlul-Bayt (AS).

Viongozi kama Aga Syed Abid Hussaini walibainisha kuwa kuunganisha Qur’an na Karbala hutoa maana nzito zaidi, na ni muhimu kwa zama hizi. Uwasilishaji wa picha za ibada za Muharram na Ilyas Rizvi uliweka wazi hisia za Azadari au maombolezo ya kidini ya Kihindi-Kashmiri, huku sanaa za kidigitali za Mubashir Hussain zikionyesha upeo wa kisasa.

Mchango wa vijana uligusa nyoyo, hususan kazi ya mtoto Syed Hyder Abbas aliyochora binti wa Imam Hussein (AS), Bibi Sakina, akimkumbatia baba yake Karbalā, ishara ya upendo na kujitolea. Wageni waliona kwamba sanaa si rangi pekee bali ni hadithi ya ndani ya moyo wa msanii.

Kwa jumla, maonyesho haya yalionekana kama jukwaa muhimu la kiutamaduni na kiroho, yakiwahimiza vijana kuelekeza ubunifu wao katika ujumbe wa milele wa Qur’an na Ashura, kumbukumbu yenye kukumbusha fadhila na uongofu wa Ahlul-Bayt (AS).

3494348

Kishikizo: kashmir ashura
captcha