IQNA

Mazungumzo serikali ya Afghanistan na Taliban mjini Doha

20:26 - September 13, 2020
Habari ID: 3473166
TEHRAN (IQNA) - Mazungumzo ya kutafuta suluhu na amani kati ya wawakilishi wa serikali ya Afghanistan na kundi la Taliban yalianza jana Jumamosi katika mji mkuu wa Qatar, Doha.

Mkutano wa mjini Doha baina ya mirengo ya Waafghani ni wa kwanza wa aina yake kufanyika nchini Qatar.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Afghanistan, hakikisho la usitishaji vita na kulinda mfumo wa jamhuri na katiba ya nchi ni miongoni mwa masuala yatakayotiliwa mkazo na ujumbe wa serikali katika mazungumzo na kundi la Taliban. Pamoja na hayo, mazungumzo ya kusaka amani baina ya Waafghani yalianza hapo jana huko nchini Qatar huku wataalamu wa mambo wakiwa na mitazamo miwili inayotafautiana kuhusu hatima na matokeo ya mazungumzo hayo.

Mazungumzo ya amani ya mjini Doha baina ya mirengo ya Afghanistan yalianza hapo jana huku suala la kulinda mfumo wa jamhuri na katiba vikiwa ndio mstari mwekundu kwa ujumbe wa serikali ya Kabul katika mazungumzo hayo. Wakati huohuo usitishaji vita ni miongoni mwa masuala muhimu yanayotiliwa mkazo na wawakilishi wa serikali ya Kabul katika mazungumo ya Doha. Hata hivyo baadhi ya wataalamu wa mambo wanasema, Taliban hawatokubali kirahisi kusitisha mapigano kwa sababu kwao wao vita ni silaha wa wenzo wa kutoa msukumo wa kupatia ushindi katika mazungumzo hayo na katika diplomasia yake.

Ukiondoa hofu na matumaini yaliyopo kuhusu mazungumzo ya amani ya Doha, ikiwa pande husika katika mazungumzo hayo zitaheshimu msingi wa jamhuri na katiba ya nchi, mchakato huo wa kuleta suluhu na amani unaweza ukawa mwanzo wa mwisho wa vita nchini Afghanistan na utangulizi wa kuondoka moja kwa moja majeshi ya kigeni katika ardhi ya nchi hiyo.

3472533

Kishikizo: afghanistan ، taliban ، doha
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :