IQNA

Hossein Amir-Abdollahian

Iran haiutambui rasmi utawala ulioko madarakani Afghanistan hivi sasa

16:42 - May 26, 2023
Habari ID: 3477050
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haiutambua mfumo wa serikali unaoongoza hivi sasa nchini Afghanistan.

, Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alisema hayo jana Alkhamisi katika mazungumzo yake na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Sayyid Hassan Khomeini, mjukuu wa Imam Khomeini (MA), katika Haram ya muasisi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu hapa Tehran.

Amesema, "Hatutambui taasisi inayotawala hivi sasa Afghanistan, na tunasisitiza juu ya haja ya kuundwa serikali jumuishi katika nchi hiyo, kwa kuwa Taliban ni sehemu tu ya uhalisia (wa mambo) nchini Afghanistan."

Aidha Amir-Abdollahian amesema Tehran imefanya mazungumzo na mamlaka za Afghanistan kuhusu mgao wa Iran wa maji ya Mto Hirmand, na kwamba Iran inaamini kuwa suala hilo linaweza kupatiwa ufumbuzi kupitia Mkataba wa 1973.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza bayana kuwa: Tumeziambia mamlaka za Afghanistan kuwa suala la sehemu ya maji ya Iran (katika Mto Hirmand) katu haliwezi kutatuliwa kupitia tu taarifa za kisiasa, lakini kupitia fremu ya sheria.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Mapatano ya Helmand yaliyosainiwa Februari 20 mwaka 1973 yameainisha wazi haki ya Iran ya kustafidi na sehemu yake ya maji ya mto huo.

Hata hivyo kutokana na kuathiriwa na mashinikizo na chokochoko za ndani na nje, serikali mbalimbali za Afghanistan zimekwepa kutekeleza wajibu wao wa kudhamini haki hiyo ya Iran.

4143483

captcha