Likitoa taarifa siku ya Ijumaa, baraza hilo limewatakia mashahidi hao hadhi ya juu na waliojeruhiwa ahueni ya haraka, huku likitoa salamu za rambirambi kwa familia zilizoomboleza.
Baraza hilo "kwa mara nyingine tena linatoa wito kwa maafisa wa usalama wa Imarati ya Kiislamu kuwakamata mara moja wahusika wa uhalifu huu wa kutisha na kuwafikisha mbele ya sheria kwa matendo yao ya aibu."
"Kwa bahati mbaya, kujirudia kwa matukio hayo ya kutisha nchini kunaonyesha kwamba, licha ya baadhi ya madai, mfululizo wa vitendo vya kikatili vya kuua watu wasio na hatia unaendelea," baraza la Shia liliongeza.
"Bila shaka, ni jukumu dhahiri la serikali kukabiliana kwa umakini zaidi na ukosefu huu wa usalama," ilionyesha taarifa hiyo
Raia takribani 14 waمهuawa katika shambulizi la kigaidi la kundi la Daesh nchini Afghanistan ambapo walikuwa wamekusanyika kuwakaribisha wafanyaziara wanaowasili kutoka maeneo matakatifu mjini Karbala, Iraq.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Afghanistan, shambulio hilo lilitokea Alhamisi saa sita mchana katika eneo la Karyudal, ambalo liko kwenye mpaka kati ya mikoa ya Daykundi na Ghor.
Ripoti zinaonyesha kuwa waliouawa ni Waislamu wa madhehebu ya Shia kutoka wilaya ya Sang Takht katika mkoa wa Daykundi, ambao walikuwa wamesafiri hadi Karyudal kukutana na jamaa zao wa kabila la Hazara waliokuwa wakirejea kutoka ziyara katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq.
Magaidi wakufurishaji wa kundi la Daesh Khorasan walilidai kuhusika na shambulio hilo.
Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaunda kundi la wachache nchini Afghanistan ambao wengi wao wanatoka katika jamii ya Wahazara nchini humo.
Mashia ni takriban asilimia 22 ya watu wa Afghanistan na wamekuwa wakidhulumiwa na kulengwa katika matukio kadhaa makubwa ya utekaji nyara na mauaji. Magaidi wakufurishaji wa Daesh wamekuwa wakitekeleza mashambulizi dhidi ya Mashia kote Afghanistan katika siku za nyuma.
3489887