IQNA

Walowezi wa Kizayuni wauhujumu Msikiti wa Al Aqsa

20:35 - September 20, 2020
Habari ID: 3473187
TEHRAN (IQNA)- Makumi ya walowezi wa Kizayuni wenye misimamo ya kufurutu ada, wakisaidiwa na polisi ya utawala wa Israel, wameuuhujumu Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo.

Katika hujuma hiyo iliyotekelezwa kwa kisingizio cha maadhimisho ya siku kuu ya Kiyahudi ya Rosh Hashanah, Wazayuni waliuhujumu msikitit wa Al Aqsa mapema leo asubuhi na kutekeleza ibada zao huku wakitekeleza vitendo vyenye kuumiza hisia za Waislamu.

Mara kwa mara wa Kizayuni huuvamia Msikiti wa al-Aqswa  wakisaidiwa na askari wa jeshi la utawala haramu wa Israel na kuuvunjia heshima msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.

Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za kukabiliana na vitendo hivyo.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Msikiti wa al-Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu umekuwa ukiandamwa na njama mtawalia za utawala vamizi wa Israel, hatua ambazo zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

/3472604

Kishikizo: wazayuni ، aqsa ، msikiti ، palestina
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :