IQNA

Sheikh Attar, Mfasiri na Hafidh wa Qur’ani Syria aaga dunia

11:16 - September 24, 2020
Habari ID: 3473199
TEHRAN (IQNA) – Sheikh Nuruddin Attar, mfasiri na hafidh maarufu wa Qur’ani Tukufu nchini Syria ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 83.

Marhum Sheikh Attar ambaye  pia alikuwa faqihi na mwanafasihi  alifariki mapema wiki hii. Alizaliwa mwaka 1937 mjini Halab au Aleppo na alimaliza shule ya upili mwaka 1954 na kisha akaelekea nchini Misri kuendeleza masomo katika Chuo Kikuu cha Al Azhar.

Alihitimu mwaka 1964 akiwa na Shahda ya Uzamivu (Ph.D) katika tafsiri ya Qur’ani na Haditihi. Alirejea nchini Syria na kuanza kufunza katika shule ya upili na kisha akaelekea Saudi Arabia kufunza Hadithi katika Chuo Kikuu cha Madina kabla ya kurejea Syria mwaka 1967.

Marhum Sheikh Attar alifunza katika vyuo vikuuu kadhaa vya nchi za Kiislamu duniani na ameandika idadi kubwa ya makala na vitabu kuhusu tafsiri ya Qur’ani, Hadithi na Fiqhi.

3924988

captcha