IQNA

Wanafunzi wa Chuo cha Kuhifadhi Qur'ani wahitimu Idlib, Syria

15:09 - November 01, 2018
Habari ID: 3471726
TEHRAN (IQNA)- Wanafunzi wa Chuo cha Kuhifadhi Qur'ani Tukufu cha Idlib, Syria wamehitimu katika sherehe ambayo iliashiria kurejea hali ya kawaida katika baada ya eneo hilo kukumbwa kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa tovuti ya al-Diyar, katika sherehe hizo za Jumanne, wanafunzi 26 waliohifadhi Qur'ani wametunukiwa zawadi. Sherehe hizo zimefanyika katika kijiji cha Atta nje kidogo ya mji wa Idlib.

Wanafunzi hao ambao walikuwa baina ya umri wa miaka 13 hadi 35 waliweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu katika kipindi cha miezi minne.

Harakati za Qur'ani nchini Syria zimeendelea pamoja na kuwa nchi hiyo ilitumbukia katika vita vilivyoibuliwa na magaidi wakufurishaji mwaka 2011.

3760055

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha