IQNA

19:41 - July 02, 2021
News ID: 3474063
TEHRAN (IQNA)- Sinan, msanifu wa majengo maarufu alichora ramani ya Msikiti adhimu wa Süleymaniye kufuatia agizo la mmoja kati ya watawala wakuu katika zama za ufalme wa Othmaniya.

Msikiti wa Süleymaniye ulijengwa kufuatia amri ya Sultan Sulaiman al-Qanuni mfalme wa 10 wa silsila wa ufalme wa Othmaniya na ulifunguliwa Oktoba 15 mwaka 1557.Msikiti huo wa kale hadi sasa umedumisha jengo lake asili na ni kati ya nembo za mji wa Istanbul.

Wengi wanaamini kuwa msikiti huu ni kati ya athari muhimu zaidi za Kihistoria za Istanbul.

Msikiti ulijengwa kulingana na mfano wa msikiti wa Hagia Sophia na ilichukua miaka 7 kuujenga. Kwa mujibu wa baadhi ya riwaya za historia, msikiti huo ulijengwa na wafanyakazi  3,523 na dhahabu yenye thamani ya kilo 3200 iligharamia ujenzi wa msikiti huo. Halikadhalika msikiti huo una maktaba kubwa yenye malaki ya vitabu vya kale na nadra kwa lugha za Kiarabu, Kiturki na Kifarsi pamoja na lugha zingine kadhaa.

Aidha msikiti huo una jengo la makumbusho ambalo linahifadhi turathi za kale za ustarabu wa Kiislamu. Kati ya athari za kale zilizohapo ni mavazi yanayonasibishwa na Mtume Muhammad SAW na bintiye, Bibi Fatima Zahra ZA pamoja Ahul Bayt AS. Halikadhalika katika jengo hilo la makumbusho kuna misahafu inayotajwa kuwa ya zama za uhai wa Mtume Muhammad SAW.

3979566

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: