IQNA

Sheikh Mkuu wa Al Azhar kutembelea Iraq

22:24 - September 18, 2021
Habari ID: 3474311
TEHRAN (IQNA)- Sheikh Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri anatazamiwza kuitembelea Iraq mwezi ujao.

Kwa mujibu wa taarifa, Sheikh Ahmed el Tayyib atafanya ziara rasmi nchini Iraq mwezi Oktoba.  Sheikh Mkuu wa Al Azhar ameitaja Iraq kuwa ‘nchi azizi’ huku akisema kuna nukta nyingi za paoja baina ya Misri na Iraq.

Akiwa safarini Iraq atatembelea mji mkuu wa Baghdad, mji wa Erbil katika eneo lenye mamlaka ya ndani la Kurdistan, mji wa Mosul na halikadhalika mji mtakatifu wa Najaf.

Ubalozi wa Iraq mjini Cairo umetangaza kuwa kutakuwa ni shughuli kadhaa muhimu wakati Sheikhe Mkuu wa Al  Azhar atakapotembelea Iraq.

3998316

Kishikizo: iraq ، misri ، al azhar ، el tayib
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha