IQNA

Masomo ya Qur'ani

Haram ya Imam Hussein AS, yasimamia kozi ya Qur'ani Mali

12:59 - June 07, 2022
Habari ID: 3475345
TEHRAN (IQNA)- Duru ya Tano ya Kozi ya Qur'ani imefanyika nchini Mali katika kituo kimoja kinachofadhiliwa na Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein AS nchini Iraq.

Kwamujibu wa tovuti ya idara hiyo, kozi hiyo ilijumuisha misingi ya Tajwedd. Sheikh Davud Jakti, mwakilishi wa Kituo cha Uenezaji Qur'ani Tukufu Mali amesema kozi hiyo ilijumuisha wanafunzi 15 kutoka vyuo vikuu mbali mbali Mali.

Tovuti hiyo inasema kozi hiyo ilifanyika kwa muda wa miezi minne na nusu na ilijumuisha harakati kadhaa za Qur'ani, ameongeza. Sheikh Jakti amesema tawi la kituo hicho katika mji wa Bamako ndicho kilichoandaa kozi hiyo. Mali ni nchi ya Afrika Magharibi ambayo aghalabu ya wafuasi wake ni Waislamu.

Jamhuri ya Mali ni nchi iliyo magharibi mwa Afrika na zaidi ya asilimi 90 ya wakazi wake ni Waislamu. Aghalabu ya Waislamu wa nchi hii ni Ahlul Sunna na hufuata madhehebu ya Maliki. Mashia wa kwanza katika nchi hii walikuwa ni wahajiri kutoka Lebanon.

 

 

4062276

captcha