IQNA

Kozi maalumu za Qiraa au Tilawa ya Qur’ani Tukufu nchini Mali + Picha

14:28 - September 17, 2021
Habari ID: 3474306
TEHRAN (IQNA)- Duru ya Tano ya Kozi Maalumu ya Kanuni za Tilawa ya Qur’ani Tukufu inafanyika nchini Mali kwa himaya ya Kituo cha Darul Qur’an cha Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein AS.

Kwa mujibu wa taarifa ya tovuti ya dar-alquran.org kozi hiyo inasimamiwa na kuendeshwa na Sheikh Dawud Jakti ambayo ni msimamizi wa Tawi la Mali la Kituo cha Darul Qur’an cha Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein AS.

Sheikh Jakti anasema kozi ya wakati huu, inayofanyika katika mji mkuu wa Mali, Bamako, inazingatia kanuni za tilawa ya Qur’ani Tukufu na inahudhuriwa na watu waliohitimu katika fani mbali mbali.

Aidha amesema kuna washiriki 25 katika kozi hiyo iliyoanza Septemba nne na watakaohitimu watapata cheti za kukamilisha masomo.

Sheikh Dawud Jakti amesema kozi hiyo itaendelea kwa muda wa miezi miwili ambapo kutakuwa na mihadhara miwili kila wiki.

Halikadhalika amesema baada ya kila somi washiriki wanahotimisha Qur’ani kwa nia ya kumzawadia thawabi Bibi Zainab SA.

Jamhuri ya Mali ni nchi iliyo magharibi mwa Afrika na zaidi ya asilimi 90 ya wakazi wake ni Waislamu. Aghalabu ya Waislamu wa nchi hii ni Ahlul Sunna na hufuata madhehebu ya Maliki. Mashia wa kwanza katika nchi hii walikuwa ni wahajiri kutoka Lebanon.

برپایی دوره تخصصی احکام تلاوت قرآن در مالی

برپایی دوره تخصصی احکام تلاوت قرآن در مالی

برپایی دوره تخصصی احکام تلاوت قرآن در مالی

برپایی دوره تخصصی احکام تلاوت قرآن در مالی

برپایی دوره تخصصی احکام تلاوت قرآن در مالی

 

3998059

captcha