IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran

Mapambano, Subira na Istiqama ni nukta msingi za fadhila za Imam Hussein AS

18:46 - August 05, 2022
Habari ID: 3475580
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema fadhila za msingi za harakati ya Imam Hussein AS zilikuwa ni mapambano au muqawama, subira na istiqama.

Hujjatul Islam Haj Ali Akbari amesema hayo katika hotuba za Sala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa Tehran na kubainisha kuwa, "Kile ambacho Imam Hussein (AS) alikifanya kilikuwa kitu cha kipekee, kwa kuutambulisha muqawama kwa jamii ya waumini."

Haj Ali Akbari ameeleza bayana kuwa, hii leo harakati za muqawama wa Kiislamu katika pembe mbalimbai za dunia zimebaki hai kutokana na kujitoa muhanga Imam Hussein (AS).

Imam Hussein (AS) ambaye kwa kujitolea kwake mhanga kusio na kifani aliuawa shahidi Siku ya Ashura, yaani tarehe 10 Muharram katika ardhi ya Karbala, amewaachia walimwengu wote somo kubwa la maana halisi ya kukomboka na kuwa na izza na heshima.

Katika sehemu nyingine ya hotuba zake, Imam huyo wa muda wa Swala ya Ijumaa hapa Tehran amebainisha kuwa, maafisa wa serikali ya Iran hawajaufungamanisha uchumi wa taifa hili na mazungumzo ya kuiondolea Iran vikwazo haramu.

Amesisitiza kuwa, timu ya mazungumzo ya Iran itayalinda maslahi ya taifa hili kwa nguvu zote, na kueleza kwamba, "Tunatoa mwito kwa maadui, Marekani na washiriki wengine wa mazungumzo wasithubutu kuipa Iran mtihani. Iwapo mnahitaji kufanya mazungumzo, tekelezeni masharti ya Iran na muache kujipendea makuu." 

4076080

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha