IQNA

Sura za Qur’ani Tukufu /72

Mafundisho ya Qu’ani Tukufu kuhusu Jini

19:41 - April 24, 2023
Habari ID: 3476908
Tehran (IQNA) - Majini ni viumbe vya ajabu ambavyo haviwezi kuonekana na macho yetu. Kuna hadithi nyingi na hadithi za kweli na za uwongo kuhusu majini lakini kulingana na Quran Tukufu, viumbe hawa wana baadi ya sifa zinazoshabihiana na zile za wanadamu.

Sura ya 72 ya Qur’ani Tukufu ni Surah al-Jinn. Inayo aya 28, Surah hii iko katika Juzuu ya 29 ya (sehemu) ya Quran. Sura hii ni Makki ikimaanisha kuwa iliteremshwa Makka na ilikuwa sura ya 40 aliyoteremshiwa Mtume Muhammad (SAW).

Jina la sura hii lintokana na  na kutajwa majini katika aya zake za kwanza, na pia maelezo ya kiumbe hiki mahali pengine katika Sura hii. Sehemu hii ya Quran Tukufu inasimulia hadithi ya Jinns wachache ambao walisikia kumbukumbu ya Qur’an Tukufu na kupata imani.

Surah al-Jinn inaangazia baadhi ya imani za uwongo za watu kuhusu jini na hutoa majibu kwao. Inaelezea Jini kama kiumbe cha kushangaza ambacho, kama wanadamu, ni huru kuchagua. Inabainisha kuwa jini hawezi kuonekana kwa sababu ya hali yake na kwamba katika hali ya kawaida, haiwezi kuhisi. Katika Siku ya Kiyama, vitendo vya majini katika ulimwengu huu pia vitapimwa.

Mada kuu ya Sura hii ni Tauhidi yaani ibada iliyotakasika ya Mungu Mmoja na kukataa kuabudu kitu kingine chochote isipokuwa Mwenyezi Mungu.

Surah inahusu vikundi viwili vya majini makafiri na wanaoamini. Pia inasisitiza kwamba Mtukufu Mtume aliwaalika majini na wanadamu kwa Uislamu.

Kulingana na Sura hi, mara tu majini waliposikia aya za Qur’ani waliona sifa yake ya kuongoza na hivyo wakaiamaini. Lakini wanadamu makafiri waliposikia aya zile zile, walimkataa Mwenyezi Mungu na walimkana Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na kumaja kuwa ni mshairi na mwendawazimu.

Mahali pengine, Sura hii inaashiria njia ambazo Mwenyezi Mungu hujaribu watu wakati pia akisisitiza hitaji la kuabudu na kumshukuru Mungu Mwenyezi. Pia inalaumu makafiri kwa kuwa na kiburi mbele ya Mwenyezi Mungu.

Mwisho wa sura, imeashiiriwa kuhusu maarifa ya Mwenyezi Mungu na nia yake ya kutoa maarifa haya kwa yeyote anayetaka.

Kulingana na aya hizo, maarifa ni ya Mungu na wengine tu wanaweza kuyapata kupitia mapenzi ya Mwenyezi Mungu na mwongozo wake.

Kishikizo: AYA ZA QURANI al jinn
captcha