IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /70

Sura Al-Ma’arij; Maelezo ya adhabu itakayotokea

16:14 - April 12, 2023
Habari ID: 3476853
TEHRAN (IQNA) – Adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa madhalimu na wakanushaji Mungu iko karibu na iko karibu zaidi kuliko wanavyofikiri. Bila shaka adhabu hiyo itajiri na hakuna kitu kinachoweza kusimama katika njia yake.

Hii ni kwa mujibu wa Surah Al-Ma’arij ya Quran Tukufu. Ni Sura ya sabini ya Qur'ani Tukufu ambayo ina Aya 44 na iko katika Juzuu ya 29. Ni Makki na ni Sura ya 79 iliyoteremshwa kwenye moyo wa Mtukufu Mtume Muhammad.

Jina la Sura linatokana na neno Ma’arij (daraja) katika Aya ya tatu. Katika aya hii, Mungu ameelezewa kuwa ni Mola wa Ma’arij (nafasi zilizotukuka, njia za kupandia).

Sura imeanza na kisa cha mtu aliyemwomba Mungu amwadhibu. "  Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea." (Aya ya 1)

Kisha inaeleza baadhi ya vipengele vya Siku ya Kiyama na baadhi ya masharti ya waumini na makafiri siku hiyo, kabla ya kuwaonya washirikina na makafiri.

Mada kuu ya sura hii ni ufufuo na Siku ya Hukumu. Inaeleza siku hiyo na adhabu zinazowangoja makafiri. Inasisitiza kwamba adhabu ni ya hakika na hakuna kinachoweza kuizuia. Sura pia inasisitiza kwamba adhabu iko karibu na haiko mbali kama wanavyofikiri makafiri.

Surah Al-Ma’arij inaweza kugawanywa katika sehemu nne kulingana na mada: Sehemu ya kwanza inazungumzia kuhusu adhabu inayokaribia kwa mtu ambaye alikanusha baadhi ya maneno ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW). Sehemu ya pili inaelezea baadhi ya vipengele vya Siku ya Hukumu na hali ya makafiri siku hiyo. Sehemu ya tatu inahusu baadhi ya vipengele vya Siku ya Kiyama na sifa za watu wema na waovu zinazowapeleka peponi au motoni. Na sehemu ya nne inajumuisha vitisho na maonyo kwa washirikina na makafiri wanaomkanusha Mwenyezi Mungu na maneno ya Mtume Muhammad (SAW). Pia inarejea tena Siku ya Hukumu.

Ama kuhusu mtu aliyemuomba Mwenyezi Mungu amuadhibu, wafasiri wa Qur'an wanasema alikuwa ni mtu aliyeitwa Numan ambaye alimpinga Mtukufu Mtume Muhammad (SAW), akisema: "Ulituita kwenye tawhidi, kuukubali utume wako, kuhiji, Jihadi, na Swalah , kufunga na kutoa sadaka, na tukazikubali. Lakini kama hayo hayakutosha unamteua kijana kuwa kiongozi wetu. Je, hili ni wazo lako mwenyewe au ni agizo kutoka kwa Mungu?” Mtukufu Mtume (SAW) alisema ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mwanamume huyo alisema kwamba ikiwa ndivyo, “Nataka Mungu anirushe juu yangu jiwe kutoka mbinguni na kunifanya nipate maumivu makali na mateso.” Wakati huo jiwe likaanguka juu yake kutoka mbinguni na kumuua. Kisha baadhi ya aya za Surah Al-Ma’arij ziliteremshwa kwa Mtukufu Mtume (SAW).

captcha