IQNA

Harakati za Qur'ani

Vikao vya Qur'ani vyafanyika Misikitini Misri

15:28 - February 28, 2024
Habari ID: 3478426
IQNA - Wizara ya Wakfu ya Misri iliandaa kongamano la Qur'ani katika misikiti 66 kote nchini.

Matukio hayo yalilenga kukuza elimu ya Qur'ani na usomaji wa Qur'ani, kwa mujibu wa wizara hiyo.

Misikiti mikubwa katika miji tofauti iliandaa kongamano chini ya kaulimbiu ya "Fadhila za Qur'an: Bora miongoni mwenu (Waislamu) ni wale wanaojifunza Qur'ani na kuifundisha".

Wizara hiyo ilisema programu hizo ni sehemu ya juhudi zinazolenga kueneza mafundisho ya Qur'ani na kuimarisha fikra za Kiislamu, tovuti ya Youm7 iliripoti.

Wizara ya Wakfu ya Misri imepanua na kubadilisha programu zake za Qur'ani katika misikiti na vituo vya kidini mwaka huu.

Programu nyingi mpya zimeundwa na kufanywa kwa ajili ya wanawake, vijana na watoto nchini.

Pia imeandaa mashindano mbalimbali ya Qur'ani kwa makundi ya rika tofauti katika ngazi za ndani, kitaifa na kimataifa.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100.

Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.

Shughuli za Qur'ani ni mashuhuri sana kutokana na kuwa maqari wakuu wa ulimwengu wa Kiislamu ni Wamisri.

3487363

captcha