Wajibu wa wizara za wakfu katika kukuza kanuni na maadili ya udhibiti ndio mada ya mkutano wa mwaka huu.
Kikao hicho kimeandaliwa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu , Dawah, na Mwongozo Saudia Arabia.
Mawaziri wa wakfu, mamufti , na wakuu wa taasisi za Kiislamu za wakfu kutoka nchi 62 wanashiriki katika hafla hiyo ya siku mbili.
Majopo mbalimbali yamepangwa kujadili masuala tofauti ya mada kuu ya mkutano huo pamoja na mambo mengine, gazeti la Okaz liliripoti.
Kukabiliana na misimamo mikali na ugaidi na kuzuia misimamo mikali katika mahubiri, maadili ya kawaida ya binadamu ya kuishi pamoja na kuvumiliana, kadhia ya chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu, kuelewa mazungumzo ya kidini na nafasi yake katika kukuza misimamo ya wastani na uimarishaji wa maadili, na hatari za kutoa Fatwa bila ujuzi sahihi ni baadhi ya mada ya kushughulikiwa katika majopo mbali mbali
Wazungumzaji pia watazungumza kuhusu vitisho vya uzushi au bidaa na njia za kukabiliana nayo, matumizi ya vyombo vya habari vya wizara za wakfu na kuzuia vitisho vinavyoletwa na vyombo vya habari na uzoefu wa wizara za wakfu katika ujenzi na utunzaji misikiti.
4229965