Mohamed Izzat, katibu mkuu wa Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu la wizara hiyo, alisema vituo hivyo vitazinduliwa katika miji kote Misri.
Aliyasema hayo katika hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa 15 wa kitamaduni wa maimamu wa swala misikitini Misri.
Amesisitiza kuwa wizara ya Awqaf ina mipango mingi ya kuendeleza shughuli za Qur'ani hususan kwa kuanzisha vituo vya kufundishia kuhifadhi na kusoma Qur'ani, tovuti ya al-Masri al-Yawm imeripoti.
Maendeleo ya mashindano ya Qur'ani katika ngazi ya kitaifa na kimataifa pia yamo kwenye ajenda, aliongeza.
Kuzindua na kupanua programu za kuhifadhi Qur'ani mtandaoni na kutengeneza programu za kufundisha Qur'ani kwa watoto ni miongoni mwa mipango mingine ya wizara hiyo, alisema.
Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100.
Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.
Shughuli za Qur'ani zimeenea sana katika nchi hii ya Kiislamu ambayo imetoa baadhi ya maqari bora zaidi wa Qur'ani duniani.
3488578