IQNA

Mchezaji Kandanda wa Uganda Travis Mutyaba Asilimu

18:42 - July 12, 2024
Habari ID: 3479110
IQNA - Mchezaji wa soka katika ngazi ya kimataifa wa Uganda Travis Mutyaba ametangaza kusilimu.

Mutyaba, ambaye anachezea Zamalek ya Misri baada ya kujiunga na timu hiyo Januari mwaka jana, alitoa tangazo hilo siku ya Jumanne. 

Alisema amebadilisha jina lake la kwanza na kuwa Jamal baada ya kusilimu, Al Jazeera imeripoti

Wachezaji wenzake walifurahia  hatua hiyo, wakimpongeza kwa kuwa Muislamu.

Mohamed Ashraf, winga wa Zamalek, aliandika katika chapisho kwenye ukurasa wake wa Instagram: "Karibu katika Uislamu ndugu yangu Jamal."

Tangu ajiunge na Zamalek, Mutyaba amekuwa na kiwango kizuri  cha uchezaji akipokea sifa kutoka kwa mashabiki.

Ndiye mchezaji wa hivi punde zaidi kati ya wachezaji wa soka wa Kiafrika waliosilimu baada ya kucheza nchini Misri.

Miongoni mwa wengine ni nyota wa Zamalek marehemu, Quarshie, pamoja na nyota wa zamani wa Al-Ahly na Zamalek, Felix Aboagye, ambaye alikuwa amebadilisha jina lake na kuwa Ahmed Felix.

 

3489101

 

captcha