IQNA

Somaliland: Mradi wa Pamoja wa Utawala wa Kizayuni na UAE

15:02 - January 01, 2026
Habari ID: 3481748
IQNA-Hatua ya kichokozi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kutambua eneo la Somalia la 'Somaliland' kama nchi huuru kunahusishwa na mradi mpana zaidi wa kuchora upya ramani ya ushawishi katika Pembe ya Afrika na Bahari Nyekundu, mradi unaoendeshwa kwa misukumo ya kiusalama kwa ushirikiano wa utawala wa Israel na pia Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Kutambuliwa kwa “Somaliland” na utawala wa Kizayuni kunahusishwa na mradi mpana zaidi wa kuchora upya ramani ya ushawishi katika Pembe ya Afrika na Bahari Nyekundu, mradi unaoendeshwa kwa misukumo ya kiusalama na kwa ushawishi wa Tel Aviv na Abu Dhabi.

Kwa mujibu wa ripoti ya IQNA, Luqman Abdullah ameandika katika gazeti la al-Akhbar la Lebanon kwamba hatua ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel, ya kulitambua eneo la Somaliland ni kilele cha historia ndefu na tata ya uhusiano wa kificho uliojengeka nyuma ya pazia. Hatua hii imewekwa ndani ya muktadha wa mradi wa kikanda wa kuchora upya ramani ya ushawishi katika Pembe ya Afrika na Bahari Nyekundu, ikihudumia maslahi ya Tel Aviv na washirika wake wa karibu, hususan Abu Dhabi.

Kwa hakika, hatua ya Israel haiwezi kutenganishwa na harakati zinazoongezeka za UAE katika eneo hilo, iwe ni kupitia msaada kwa udhibiti wa Baraza la Mpito la Kusini katika mashariki mwa Yemen, au kwa nafasi zisizo za moja kwa moja nchini Sudan.

Muundo mpya wa kijeshi na kisiasa

Mabadiliko katika maeneo haya, ingawa kwa nje yanaonekana kutofautiana, kwa hakika yanakaribiana zaidi na uwanja mmoja wa kiutendaji ambapo Israel, kwa kushirikiana na UAE, imechukua jukumu la kuongoza juhudi za muunda mpya kijeshi na kisiasa.

Hili limeelezwa kwa uwazi katika ripoti ya kituo cha Kizayuni cha lugha ya Kiarabu i24News, kilichonukuu vyanzo vya habari vilivyofichua ushiriki wa Umoja wa Falme za Kiarabu katika mazungumzo yaliyosababisha hatua ya Israel ya kuitambua Somaliland.

Ansarullah ya Yemen

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, shirika la kijasusi la Israel (Mossad) kwa miaka mingi limekuwa likishirikiana kwa njia ya kificho na Somaliland, mbali na vyombo vya habari vya umma au uwakilishi wa kidiplomasia, ikijumuisha uratibu wa kijasusi, makubaliano ya kiusalama na maandalizi ya kisiasa kwa ajili ya kutambuliwa rasmi.

Hatua ya hivi karibuni imekuja sambamba na wasiwasi unaoongezeka wa Israel kuhusu kuimarika kwa uwezo wa kijeshi wa Ansarullah nchini Yemen, hususan katika nyanja za makombora, ndege zisizo na rubani (drones), na vitisho vya baharini. Uwezo huu mpya umeunda uwezo wa Yemen kuzuia mashambulizi katika Bahari Nyekundu na lango la Bab al-Mandab, maeneo yenye umuhimu wa kimkakati kwa usafiri wa kimataifa na kwa Waislamu wa pwani.

Katika muktadha huu, gazeti la Kizayuni Yedioth Ahronoth linaripoti kwamba Israel, sawa na Marekani, inaipa kipaumbele Somaliland kutokana na pwani yake ndefu, nafasi yake ya kistratejia katika Pembe ya Afrika, na ukaribu wake na maeneo yanayodhibitiwa na Ansarullah nchini Yemen.

Ni vyema kutaja kwamba Amichai Chikli, Waziri wa Masuala ya Wayahudi waishio nje ya Israel, alithibitisha kuwa “hatua hii ni mafanikio makubwa katika kukabiliana na Wahouthi (Ansarullah).”

Nukta ya Mhimili

Gazeti la Maariv kwa upande wake lilieleza kuwa faida ya kutambuliwa kwa Somaliland haiko katika sura ya kidiplomasia, bali katika nafasi yake ya kijiografia. Bandari ya Berbera, iliyo kwenye pwani ya Ghuba ya Aden, pamoja na uwanja wa ndege ulio karibu , wenye moja ya njia ndefu zaidi za kutua na kuruka barani Afrika , vinalifanya eneo hilo la  Somalia kuwa katika nukta ya mhimili, ikitazama moja kwa moja moja ya njia muhimu zaidi za usafirishaji baharini duniani.

Katika muktadha huu maalum, inaonekana kwamba uamuzi wa Israel unahusiana moja kwa moja na haja ya dharura ya Tel Aviv ya kutafuta mbadala wa kistratejia ambao utaihakikisha usalama wa baharini na kulinda njia muhimu za biashara na nishati ,  hususan ikizingatiwa kupungua kwa ufanisi wa zana za kijeshi za kizamani katika kukabiliana na kuimarika kijeshi Yemen.

Aidha, hatua ya kutambua Somaliland kama nchi huru imewekwa ndani ya njama ya Israel za kupanua upeo wa ile sera ya Raist Trump wa Marekani ya “Makubaliano ya Abrahamu” ambayo yanalenga kuzilazimua nchi za Kiislamu ziwe na uhusiano na Israel. Sera hiyo sasa inatekelezwa mashariki mwa Afrika , hata kupitia tawala ambazo hazijatambuliwa kimataifa, ili kulazimisha hali mpya za kisiasa na kiusalama katika eneo hilo na kuondoa mipangilio yoyote ya kikanda ambayo ingeweza kuiondoa Israel kutoka mahesabu ya kimkakati katika Bahari Nyekundu na Pembe ya Afrika.

Misri, Saudia na Uturuki zinalengwa

Ahmed Davutoğlu, Waziri Mkuu wa zamani wa Uturuki, amesema hatua ya Israel kutambua Somaliland ni shambulio la moja kwa moja dhidi ya maslahi ya Misri, Saudi Arabia na Uturuki katika eneo. Aliongeza kuwa ni sehemu ya mkakati mpana zaidi wa kugawa nchi za Kiislamu na kudhoofisha mataifa muhimu kwa kuyazingita.

Israel, si tu inalenga kugawa Somalia au kuchochea vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vinaweza kushuhudia maafa makubwa sawa na yanayotokea Sudan, bali pia inakusudia kupata ufikiaji wa Bandari ya Berbera , bandari ya kistratejia na muhimu iliyo katika lango la Bahari Nyekundu kwenye Ghuba ya Aden. Hatua hii kwa hakika itazizingira Misri, Saudi Arabia na pia Uturuki, ambayo ina kituo cha kistratejia muhimu nchini Somalia na ambacho ni cha lazima kwa siasa zake kuelekea bara la Afrika.

Hivyo basi, nchi za Kiarabu na Kiislamu mlicha ya tofauti zao kali ,  zilitoa kwa haraka tamko la pamoja lililopinga hatua ya Israel, na hivyo kuonyesha ufahamu wa pamoja kuhusu athari za kisiasa na kimuundo kwa maslahi yao ya pamoja.

Nchi zilizotia saini tamko hilo zilijikuta zikikabiliana na historia hatari inayotishia kanuni ya umoja wa dola na kufungua mlango wa kuhalalisha tawala za kujitenga. Njia hii inaleta athari za moja kwa moja kwa uthabiti wa eneo zima na ni onyo kuhusu uwezekano wa kutumiwa kwa migawanyiko ya ndani katika nchi dhaifu ili kuondoa mshikamano wao.

Kwa upande mwingine, haikuwa jambo la kushangaza kwamba Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Bahrain zilikataa kujiunga na tamko hilo. Nafasi yao imefungamana moja kwa moja na miradi inayolenga kubadilisha sura ya eneo kwa mujibu wa maono ya “Mashariki ya Kati Mpya” ambayo Netanyahu amekuwa akiunga mkono daima.

Ni vyema kutaja kwamba UAE hapo awali ilijaribu kufanikisha juhudi za kulitambua Somaliland kimataifa kupitia Umoja wa Mataifa, lakini juhudi hizo ziligonga mwamba na zikashindwa.

Bandari za Somalia

Juhudi hizi zilikuwa sehemu ya mkakati mpana zaidi wa Umoja wa Falme za Kiarabu wa kujenga “Satwa Ushawishi” inayotegemea udhibiti wa bandari na njia muhimu za maji , ikiwemo Bahari Nyekundu na Ghuba ya Aden , pamoja na vituo vya kijeshi na kuhakikisha usalama wa njia za biashara na nishati za kimataifa kwa uratibu na Marekani na Israel.

Kwa kuzingatia kwamba mkakati wa UAE unategemea makampuni ya bandari ya Dubai na Abu Dhabi, ambayo hufanya kazi kama mikono ya kibiashara na kistratejia ya taifa hilo, nchi imefanikiwa kudhibiti mtandao wa bandari muhimu unaoenea kote Afrika na katika Rasi ya Kiarabu.

Katika muktadha huu, uwekezaji wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) katika Somaliland unaonyesha hamu ya Abu Dhabi ya kuthibitisha nafasi yake katika muunda wa kiusalama na kiuchumi kikanda, ambapo maslahi ya yake yanakutana na yale ya utawala wa Israel.

Miongoni mwa vipengele vinavyojitokeza zaidi katika uwekezaji huu ni matumizi ya zaidi ya dola milioni 442 kwa ajili ya kuendeleza Bandari ya Berbera (Somaliland) na kuibadilisha kuwa kituo cha kijeshi na cha kisasa cha usafirishaji, bila ushirikiano wowote na serikali ya shirikisho mjini Mogadishu. Aidha, Bandari ya Bosaso (Puntland) imegeuzwa kuwa kitovu kingine cha kistratejia nchini Somalia, nacho pia kikiwa huru na mamlaka ya serikali kuu.

/4325875

captcha