IQNA

Tamasha la 19 la Kimataifa la Filamu za Muqawama (Mapambano)

15:49 - November 30, 2025
Habari ID: 3481594
IQNA-Tamasha la 19 la Kimataifa la Filamu za Muqawama au Mapambano litafanyika kuanzia Mei 17–23, 2026, mjini Tehran na mikoa mingine ya Iran.

Tamasha hili litaandaliwa na Jumuiya ya Mapinduzi na Ulinzi Mtakatifu chini ya uongozi wa Jalal Ghaffari Ghadir.

Sherehe ya kuwatunuku na kuwaheshimu washindi wa tamasha hili itafanyika Mei 24, 2026, sambamba na Siku ya Muqawama, Kujitolea na Ushindi.

Wito wa kushiriki katika toleo la 19 la tamasha umetolewa na Sekretarieti ya Kudumu ya tamasha.

Sehemu kuu ya tamasha itajumuisha filamu ndefu, filamu fupi, makala (documentaries), katuni (animations), miswada ya filamu (screenplays), na utafiti na ukosoaji wa sinema ya mapambano na masuala ya kibinadamu.

Sehemu ya ziada ya tamasha itajumuisha kazi za akili bandia na nyenzo za matangazo.

Wanaotaka kushiriki wanaweza kuwasilisha kazi zao kwa Sekretarieti ya Kudumu ya Tamasha la Kimataifa la Filamu za Mapambano kwa kujaza fomu ya usajili wa kazi kuanzia Novemba 29, 2025 hadi Februari 19, 2026 kwa makala, filamu fupi, katuni, miswada, kazi za akili bandia, nyenzo za matangazo, utafiti, ukosoaji, tasnifu na vitabu, na hadi Machi 11, 2026 kwa filamu ndefu.

Kazi zitakubaliwa tu kupitia tovuti rasmi ya tamasha www.resistanceiff.com na sekretarieti ya tamasha iko mtandaoni kikamilifu kupokea kazi kutoka kwa watengenezaji filamu, wasanii na wanaharakati wa sinema ya mapambano.

3495564

Kishikizo: tamasha filamu muqawama
captcha