IQNA

Iran kuendelea kuunga mkono mapambano ya Wapalestina

16:05 - August 29, 2024
Habari ID: 3479348
IQNA-Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inaunga mkono makubaliano yoyote ambayo yanakubaliwa na Wapalestina na muqawama.

Sayyid Abbas Araghchi amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Khalil al-Hayy, mjumbe wa ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na kusisitiza kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaunga mkono makubaliano yoyote ya usitishaji vita na kuhitimisha vita vya Gaza ambavyo yanakubaliwa na wananchi wanamuqawama wa Palestina, makundi ya muqawama na harakati ya Hamas.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amepongeza kusimama kidete kwa watu wa Gaza na muqawama wa miezi 11 dhidi ya jinai za Wazayuni, na kueleza imani yake kuwa ushindi wa mwisho utakuwa wa wananchi wa Palestina na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakuwa upande wao hadi mwisho.

Kwa upande wake Khalil Al-Hayya, mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa na anayehusika na mahusiano ya Kiarabu na Kiislamu katika Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ampongeza Abbas Araghchi kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Al-Hayya amepongeza juhudi za shahidi Waziri Amir Abdullahian katika kuunga mkono muqawama wa wananchi wa Palestina, na kusisitiza: Wananchi wa Palestina wanathamini uungaji mkono endelevu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa wananchi wa Wapalestina na muqawama wake dhidi ya jinai za Wazayuni.

3489686

Habari zinazohusiana
captcha