IQNA

Usomaji Qur'ani Tukufu nchini Misri

Mwanafunzi wa Al-Azhar ni Qari mchanga Zaidi wa Televisheni na Redio ya Misri

16:54 - December 14, 2023
Habari ID: 3478035
IQNA - Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar alijiunga rasmi na Televisheni na Redio ya Misri kama qari mwenye umri mdogo zaidi.

Abdul Razaq al-Shihawi ni qari aliyeshika nafasi ya tatu katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Katara ya Qatar mapema mwaka huu.

Pia ameshinda nafasi ya juu kabisa katika mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Misri, kwa mujibu wa tovuti ya Cairo24.

Al-Shihawi ameshukuru kwa uteuzi huo, akisema ilikuwa ndoto yake tangu utotoni.

Alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa mafanikio hayo na huku akisema ameweza kufika alipo kutokana na himaya ya familia yake, walimu na wananchi.

Al-Azhar Student Becomes Youngest Qari of Egypt’s TV & Radio    

Al-Shihawi ameathiriwa katika usomaji wake na maqari wakubwa kama Sheikh Mustafa Ismail, Sheikh Abdul Basit Abdul Samad na Sheikh Khalil al-Husari.

Pia husikiliza sana visomo vya Qur'ani vya Sheikh Muhammad Shahat Anwar na kuiga mtindo wake.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100. Waislamu wanachukua karibu asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo. Shughuli za Qur'ani ni maarufu sana katika nchi za Kiarabu zenye Waislamu wengi. Idadi kubwa ya maqari au wasomaji bora wa Qur'ani Tukufu katika ulimwengu wa Kiislamu ni kutoka misri

Kilpi hii ina mojawapo ya visomo vya Qur'ani vya Sheikh al-Shihawi:

 

 

3486419

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qari misri
captcha