IQNA

Uchambuzi

Utawala wa Israel unajaribu sana kusambaratisha mhimili wa Muqawama

20:13 - December 07, 2024
Habari ID: 3479870
IQNA - Utawala wa Kizayuni wa Israel unalenga kwa nguvu zote kusambaratisha mhimili wa muqawama Asia Magharibi na kutenganisha makundi ya muqawama huko Iraq, Syria na Lebanon, amesema mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Iraq.

Ali Nasser ameyasema hayo katika mahojiano yake na IQNA kufuatia matukio ya hivi karibuni ya kieneo katika eneo hilo hususan nchini Syria.

Amesisitiza kwamba muqawama unaendelea kufurahia nguvu kubwa na unaweza kuendelea kufanya kazi kama chombo kimoja na kuzuia njama za adui.

Kuhusu uanzishaji wa makundi ya kigaidi nchini Syria, amesema magaidi hao wanaungwa mkono na utawala wa Israel na Marekani.

Amesema utawala wa Kizayuni ambao umekuwa ukikabiliwa na mapigo makali kutoka kwa makundi ya muqawama, umekuwa ukipanga kuuzima mhimili huo wa muqawama.

"Nadhani hali ya sasa katika kanda na kufuatia kusitishwa kwa mapigano nchini Lebanon ni muhimu sana kwa mhimili wa muqawama. Utawala wa Kizayuni kwa makusudi unataka kulisukuma eneo kuelekea vita. Hata kusini mwa Lebanon, utawala huo umekiuka makubaliano ya kusitisha mapigano. Kwa hivyo kwa sasa ni muhimu sana kusaidia na kuunga mkono mhimili wa muqawama.

Amesema nchi za Kiislamu zinapaswa kujitahidi kuzuia njama za Israel kwa eneo hilo ikiwemo ile ya Syria.

"Nchi za Kiislamu zinapaswa kuungana na kusaidia Syria katika hali ngumu ya sasa," alisisitiza.

Nasser aidha alivikosoa baadhi ya vyombo vya habari vya Kiarabu vinavyoeneza habari potofu na kuchukua hatua kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni ili kuchochea moto wa migogoro katika eneo.

"Ninaamini kuwa katika hali ya sasa, vyombo vya habari vina jukumu kubwa na vina jukumu zito kwani vinapaswa kueneza ujumbe wa amani," alisisitiza.

Syria imekuwa ikikabiliana na magaidi na wanamgambo wanaofadhiliwa na mataifa ya kigeni tangu Machi 2011, huku Damascus ikisema mataifa ya Magharibi na washirika wao wa kieneo wanayasaidia makundi hayo ya kigaidi kufanya uharibifu katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Magaidi wa  Hayat Tahrir al-Sham walianzisha mashambulizi makubwa katika majimbo ya Aleppo na Idlib kaskazini magharibi mwa Syria mnamo tarehe 27 Novemba, na kuyateka maeneo kadhaa. Tangu wakati huo, vikosi vya serikali ya Syria vimekuwa vikishiriki katika makabiliano makali ili kukomboa ardhi zilizotekwa.

3490954

Kishikizo: muqawama syria israel
captcha