IQNA

Ayatullah Mohsen Araqi

Palestina sasa itafakari kuuangamiza utawala wa Kizayuni

17:12 - September 09, 2014
Habari ID: 1448558
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu Ayatullah Mohsen Araqi ameashiria ufanisi wa mapambano ya watu wa Palestina mbele ya hujuma ya utawala wa Kizayuni katika vita vya hivi karibuni vya Ghaza.

Ameongeza kuwa, "Palestina sasa imeingia katika kipindi kipya endelevu ambapo wakati umewadia wa kung'oa mizizi ya utawala wa Kizayuni na ili kufikia lengo hilo kunahitajika ushirikiano katika Ulimwengu wa Kiislamu."

Mwanazuoni huyo ameyasema hayo katika hotuba yake kwa Kikao cha kwanza cha kimatiafa cha  'Maulamaa wa Kiislamu Wanaounga Mkono Harakati ya Muqawama' kinachofanyika Tehran, mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Ayatullah Araki amesisitiza kuhusu udharura kwa wasomi wa  Ulimwengu wa Kiislamu kutafakari pamoja kuhusu kadhia ya Palestina.  Ameongeza kuwa lengo la kongamano hilo la kimatiafa ni kuundwa  'Jumuiya ya Kimatiafa ya Maulamaa wa Muqawama' na pia kuwaleta pamoja wale wote walio tayari kuwasaidia wahanga na ukatili wa Wazayuni na Matakfiri.
Kongamano hilo la siku mbili limewaleta pamoja wasomi na maulamaa wa Kiislamu zaidi ya 200 kutoka nchi 53 kwa lengo la kuunda 'Jumuiya ya Maulamaa wa Muqawama.'

1448313

captcha