IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Muqawama unaostawi Asia Magharibi umesambaratisha ujeuri na majigambo ya ubeberu

20:50 - February 17, 2022
Habari ID: 3474937
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, muqawama (mapambano ya Kiislamu) unaokua na kuzidi kupata nguvu katika eneo la Asia Magharibi umesambaratisha kiburi na majigambo ya ubeberu.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo sambamba na kukaribia kumbukumbu ya harakati ya kihistoria ya wananchi wa Tabriz ya 29 Bahman 1356 Hijria Shamshia (18 Februari 1978) wakati alipozungumza kwa mawasiliano ya intaneti na hadhara ya wananchi wa mkoa wa Azerbaijan na kueleza kwamba, muqawama unaokua katika eneo umesambaratisha ujeuri na majigambo ya ubeberu na ndimi za mataifa zimefunguka mbele ya Marekani na kwamba, kuna haja ya kutambua thamani ya neema hii kwa kuendeleza njia ya mapinduzi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiiislamu ameongeza kuwa, malengo ya mapinduzi ni kupatikana ustawi na maendeleo ya kweli na ya pande zote za kimaada na kimaanawi, kupatikana uadilifu wa kijamii, nguvu na mamlaka ya nchi, kuundwa jamii ya Kiislamu na hatimaye kuundika ustaarabu mkubwa na wa kisasa wa  Kkiislamu.

Ayatullah Khamenei amesema, nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani ni mahitaji mengine ya kimsingi ya mustakabali na kueleza kwamba, sababu ya kambi ya adui kuegemea katika suala la nishati ya nyuklia ya Iran na kuliwekea vikwazo vya kidhalimu taifa hili licha ya kuweko taarifa zinazoonyesha kuwa, miradi ya nyuklia ya taifa hili ni kwa ajili ya matumizi ya amani na kutolewa maneno yasiyo na maana kama kukaribia Tehran kutengeneza silaha za atomiki, ni kuzuia ustawi wa kielimu ambao unalenga kukidhi mahitaji ya baadaye ya taifa hili.

4036984

captcha