IQNA

Trump analenga kukamilisha mradi wa Marekani-Uzayuni wa kuangamiza Muqawama

20:56 - February 16, 2025
Habari ID: 3480225
IQNA – Mchambuzi wa kisiasa wa Iraq alisema vita vya Gaza vilikuwa sehemu ya njama ya Marekani-Uzayuni za kuangamiza harakati za Muqawama au mapambano ya Kiislamu katika eneo la Asia Magharibi. Akizungumza katika mahojiano na IQNA kuhusu hali ya Gaza na usitishaji mapigano kati ya Hamas na utawala wa Israel, Sannan al-Saadi amesema Rais wa Marekani Donald Trump sasa anatafuta kukamilisha mradi huu.

Akitilia mkazo kwamba watu wa Palestina walitokea washindi katika vita vya Gaza, alisema kuwa licha ya kupata hasara na kutoa mashahidi wengi, Wapalestina wamebaki imara katika njia ya Muqawama. Aliongeza kuwa makubaliano ya usitishaji mapigano yalikuwa fedheha kubwa kwa utawala wa Kizayuni, lakini Benjamin Netanyahu alilazimika kuyakubali kwa sababu utawala huo ulipata hasara kubwa katika vita. Mashinikizo ya kimataifa pamoja na matatizo ya kisiasa na kiuchumi ya ndani pia yalikuwa na nafasi muhimu katika kulazimisha Tel Aviv kukubali usitishaji mapigano, al-Saadi alisema.

Alipoulizwa kuhusu maoni ya hivi karibuni ya Trump juu ya Gaza, alisema, “Sote tunajua kuna mradi wa Marekani-Uzayuni katika eneo hilo ambao ulitekelezwa Gaza, kisha kusini mwa Lebanon na Syria. Vikwazo pekee vilivyobaki kwa utekelezaji wa mradi huu ni Harakati ya Ansarullah ya Yemen na makundi ya Muqawama nchini Iraq. Kwa hivyo, tunaona kuwa Trump alikuwa mkali kuhusu kumaliza vita vya Gaza ili kisha aanzishe vita dhidi ya Ansarullah na vikundi vya Iraq, hatimaye akilenga kuleta Iran kwenye mazungumzo kulingana na masharti ya Marekani.

Al-Saad pia aliulizwa kuhusu mustakabali wa uhusiano kati ya Hamas na Mamlaka ya Palestina. Alisema hakutakuwa na mustakabali mzuri kwa uhusiano kati ya Hamas na Mamlaka ya Palestina, hasa kwa kuwa hakuna upande unaoaminiana, na kama tulivyoeleza, kuna mvutano wa kijamii na mgongano kuhusu uhalali kati ya pande hizo mbili. Ukanda wa Gaza ni kitovu cha mzozo wa siku zijazo kati ya Hamas na Mamlaka ya Palestina, aliendelea kusema.

3491867

Habari zinazohusiana
Kishikizo: gaza trump muqawama
captcha