
Sheikh Khairuddin, ambaye ni mkuu wa Dar-ul-Qur’an al-Karim chini ya usimamizi wa Haram tukufu ya Imam Hussein (AS) huko Karbala, alitoa kauli hiyo Jumanne katika hafla ya uzinduzi wa Mawsu‘ah Ahlul-Bayt al-Qur’aniyya: Ensiklopidia ya Qur’ani ya Ahlul-Bayt (AS), kazi kubwa iliyokusanywa na taasisi hiyo.
Alisema: “Ni lazima tufikie Waislamu kote ulimwenguni ili wafahamu kuwa furaha ya mwanadamu na ukombozi wake, duniani na Akhera, unategemea kufuata njia ya Mtume Muhammad (SAW) na Ahlul-Bayt wake (AS).”
Sheikh al-Hadi alifafanua kuwa ensiklopidia hii ina sura mbili: ya kwanza ni taasisi iliyosimamia uandishi wake, na ya pili ni asili ya kazi yenyewe. Alikumbusha mazungumzo yake na ndugu zake huko Mashhad, walioshangazwa kuona ensiklopidia ya kwanza ya aina hii ikichapishwa Iraq. Alisema: “Hatukuleta jambo jipya, bali tulikusanya na kuchambua kazi za Ahlul-Bayt (AS) zilizokuwapo katika vitabu vya rejea vya Kiislamu, kisha tukaziorodhesha na kuzipanga. Hii yenyewe ni khidma kubwa kwa Ahlul-Bayt.”
Aidha, alieleza kuwa baadhi ya watu hudai kuwa Ma‘sumin (AS) hawana mtazamo kuhusu Qur’ani, na hata katika vyuo vikuu baadhi ya wasomi husema hivyo. “Kwa hiyo, kazi hii ilikuwa muhimu sana katika wakati wake,” aliongeza.
Sheikh al-Hadi alisisitiza kuwa kuchapishwa kwa ensiklopidia hii chini ya kuba ya Sayyid al-Shuhada (AS) ni neema ya Mwenyezi Mungu. “Leo Imam Hussein (AS) ni wa ulimwengu mzima. Macho ya mataifa, hasa katika kutafuta urithi halisi wa Kiislamu na ubinadamu, yameelekezwa kwake. Imam Hussein (AS) ni mkombozi wa wanadamu. Watu kutoka zaidi ya nchi mia moja huja Karbala, hususan siku za Arba‘een, kunufaika na elimu na mafundisho yake.”

Aliongeza kuwa Dar-ul-Qur’an al-Karim ilianzishwa baada ya kuanguka kwa utawala wa Ba‘ath nchini Iraq, kwani awali haikuruhusiwa kujenga taasisi za Qur’ani zinazohusiana na Ahlul-Bayt (AS).
Sheikh al-Hadi alieleza malengo matatu ya Dar-ul-Qur’an:
Sheikh al-Hadi alisimulia tukio la mwanazuoni kutoka Misri aliyemuuliza: “Wanasema Shia wana Qur’ani tofauti na ile ya Sunni. Naweza kuona nakala yenu?!” Akasema: “Hata leo, mwaka 2025, licha ya majukwaa mengi ya kielimu na vyombo vya habari, bado wengi hawatufahamu, kwa sababu hawako tayari kusoma urithi wetu au kusikiliza mtazamo wa Shia. Ni wajibu wetu kuwafikia, ili watambue kuwa furaha na ukombozi wa mwanadamu duniani na Akhera uko katika kufuata njia ya Muhammad (SAW) na Ahlul-Bayt wake (AS).”
Alimalizia kwa kusema kuwa baada ya kuchapishwa kwa ensiklopidia hii, simu nyingi zilipokelewa kutoka Misri, Morocco, Libya, Algeria na nchi za Ghuba ya Uajemi, zikisema: “Kwa mara ya kwanza tunasikia kuwa Ahlul-Bayt wameeleza kuhusu Qur’ani!”

4321960