IQNA

Ayatullah Reza Ramezani

Nchi za Kiislamu ziishinikze serikali ya Nigeria imuachilie huru Sheikh Zakzaky

9:26 - December 25, 2019
Habari ID: 3472301
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt AS ametoa wito kwa nchi za Kiislamu ziishinikize serikali ya Nigeria imueachilie huru kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) Sheikh Ibrahim Zakzaky.

kikao na waandishi wa habari, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka minne, tangu lijiri tukio la wanajeshi wa Nigeria kushambulia kituo cha kidini cha Baqiyatullah na nyumba ya mwanazuoni huyo katika mji wa Zaria jimboni Kaduna kaskazini mwa Nigeria. Halikadhalika ametoa wito kwa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) kuingilia kati ili Sheikh Zakzaky aachiliwe huru.

Amebainisha kuwa, "Sheikh Zakzaky anapinga uhasama wa kimadhehebu miongoni mwa Waislamu, na ana anaamini kuwa mazungumzo ndiyo njia bora ya kuimarisha mshikamano." Aidha amemtaja Sheikh Zakzaky kuwa, mwanazuoni anayepigania umoja katika ulimwengu wa Kiislamu.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt AS sambamba na kukosoa hatua ya kuendelea kuzuilia kinyume cha sheria Sheikh Zakzaky, ameeleza bayana kuwa, taasisi anazozisimamia Sheikh Zakzaky zinawasaidia mayatima na masikini.

Ayatullah Ramezani amesema, "Nukta muhimu ambayo tunapaswa kuzingatia ni kuwa, mbali na masaibu aliyokumbana nayo Sheikh Zakzaky na matatizo mengine aliyoyapata ikiwa ni pamoja na kuuawa shahidi watoto wake na kuwepo haja ya kufuatiliwa katika taasisi za kimataifa; muhimu zaidi hivi sasa ni kuwa hali ya Sheikh Zakzaky si nzuri".  Amesema madaktari wataalamu wameonya kuwaiwapo hali yake itaendelea ilivyo hivi sasa yamkini akakumbwa na hali mbaya zaidi. Amebaini kuwa, "Hivi sasa ana risasi katika mwili wake, jicho lake moja halioni na ana maradhi mengine mengi na kwa kuzingatia hali hiyo ya Sheikh Zakzaki, taasisi za kimataifa zinaweza kuishawishi serikali ya Nigeria izingatie suala la kumpa matibabu ili afya yake irejee. Iwpao hili litafanyika basi hatakumbwa na matatizo makubwa zaidi katika afya yake siku za usoni."

Itakumbukwa kuwa, Sheikh Ibrahim Zakzaky, 66, na mkewe walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015 wakati askari wa jeshi la Nigeria walipovamia na kushambulia Hussainiyah iliyoko katika mji wa Zaria. Katika shambulio hilo, Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Nigeria wasiopungua 1,000, wakiwemo wana watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky, waliuawa shahidi.

Nchi za Kiislamu ziishinikze serikali ya Nigeria imuachilie huru Sheikh Zakzaky

Baada ya jitihada kubwa, maandamano ya kila pembe na mashinikizo mengi ya ndani na kimataifa, mnamo mwezi Agosti, mahakama ya Nigeria iliruhusu Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe wapelekwe India kutibiwa, lakini kutokana na matatizo na vizuizi vilivyowekwa na maafisa wa usalama walioandamana naye, kiongozi huyo wa kidini pamoja na mkewe waliamua kurudi Nigeria baada ya kukaa India kwa muda wa siku mbili tu pasi na kupatiwa matibabu.

Kabla ya hapo, Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ilikuwa imefichua kwamba, serikali ya nchi hiyo imekula njama ya kumuua Sheikh Zakzaky kwa kutumia mbinu tofauti ikiwemo ya kumpa sumu.

3866301

captcha