IQNA

Umuhimu wa kuichambua kadhia ya Ashura kitaalamu + Video

TEHRAN (IQNA)- Kuna umuhimu wa kuiangazia kadhia ya Siku ya Ashura kwa mtazamo wa kitaalamu na kina badala ya kufahamu tu tukio lilivyojiri.

Hayo yamesemwa na msomi wa masuala ya Ashura Dkt. Muhsin Ismaili katika mfululizo wa mihadhara yake ya mwezi huu wa Muharram.

Katika kikao chake cha kwanza, amesisitiza umuhimu kuchambua historia ya Ashura  na kuweka wazi kanuni za Mwenyezi Mungu.

Aidha amesema Qur’ani Tukufu inawataka Waislamu kuangazia matukio ya historia ili watafakari wapate ibra na funzo. Amefafanua zaidi kwa kuashiria aya ya 176 ya Surah Al A’raf katika Qur’ani Tukufu isemayo: “Na tungelitaka tungeli mtukuza kwa hizo Ishara, lakini yeye aliushikilia ulimwengu na akafuata pumbao lake. Basi mfano wake ni mfano wa mbwa. Ukimhujumu hupumua na kutoa ulimi na ukimwacha pia hupumua na kutoa ulimi. Huo ni mfano wa kaumu wanao zikanusha Ishara zetu. Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari.”

Kwa msingi huo Dkt. Ismaili amesisitiza kuhusu kutafakari kuhusu matukio ya historia kwani kufanya hivyo pia ni katika Sunnah za Mtume Muhammad SAW. Amesema tukio la Ashura pia linapaswa kutazamwa katika msingi huo wa kutafakari ili kumfahamu ujumbe wa Imam Hussein AS katika jangwa la Karbala. Amesema tunapaswa kufahamu ni kwa nini Imam Hussein AS aliuawa shahidi na malengo ya mwamko wake.

3475468

Kishikizo: imam hussein as ، ashura