IQNA

Kiongozi wa Hizbullah Awahimiza Waombolezaji wa Muharram Kuzingatia Kanuni za Afya

21:29 - August 11, 2021
Habari ID: 3474181
TEHRAN (IQNA)-Katibu mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesistiza ulazima wa wale wanaohudhuria maombolezo ya Muharram kuzingatia kanuni za kiafya.

Akizungumza kwenye hafla ya kuomboleza usiku wa kwanza wa mwezi wa Hijri wa Muharram, Sayed Hassan Nasrallah pia alisema Waislamu wanapaswa kuendelea kujitolea kwa mujibu wa mafundisho ya kidini kuhusu uvumilivu na kusimama kidete mbele ya ukandamizaji.

Waislamu nchini Lebanon walianza kufanya ibada ya kuomboleza siku ya kwanza ya Muharram jana usiku.

Katika mwezi wa Muharram Waislamu, hasa wa madhehebu ya Shia, na wapenda haki kote duniani hukumbuka  tukio la Ashura ambalo lilijiri takribani miaka 1382 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria Qamaria.

Katika tukio hilo, moja kati ya vita mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu, vilitokea baina ya majeshi ya haki na batili katika ardhi ya Karbala huko Iraq. Siku hii inajulikana kwa jina la Ashura. Katika siku hiyo mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib AS, alisimama kishujaa na wafuasi wake waaminifu 72, kukabiliana na jeshi la batili ili kuilinda dini ya Allah. Hamasa ya Karbala ilikuwa dhihirisho la mambo mawili makuu. Kwanza ni ujasiri, ushujaa, moyo wa kujitolea, uaminifu pamoja na kuyapokea kwa moyo mkunjufu mauti ya kuuawa shahidi, sifa walizojipamba nazo wapiganaji wachache wa jeshi la haki wakiongozwa na Imam Hussein AS dhidi ya Yazid bin Muawiya.

3989653

Kishikizo: nasrallah muharram
captcha