IQNA

"Kila siku ni Ashura na kila ardhi ni Karbala" + Video

TEHRAN (IQNA)- Kuna msema usemao "Kila siku ni Ashura na kila ardhi ni Karbala." Lakini maana yake ni nini haswa?

Akizungumza katika mfululizo wa vikao vyake kuhusu Ashura, Dkt. Muhsin Ismaili amefafanua zaidi kuhusu tukio la Ashura.

Katika kikao chake cha tatu amesema msemao usema "Kila siku ni Ashura na kila ardhi ni Karbala," si hadithi kama wengine wanavyodhani bali ni msemo wa hekima.

Amesema maana ya msema huo ni kuwa, sisi katika maisha yetu duniani na pumzi tunayopumua ni Karbala yetu. Ameongeza kuwa, sisi pia, popote tulipo na wakati wowote ule, tuko katika mapmabano na tunapaswa kuamua iwapo tutajiunga na Jeshi la Imam Hussein AS na kufuata njia ya haki au, Mungu aepushe, tujiunge na jeshi la Omar Saad, yaani kuwasaidia madhalimu na watenda maovu katika zama hizi.

Katika mwezi wa Muharram Waislamu, hasa wa madhehebu ya Shia, na wapenda haki kote duniani hukumbuka  tukio la Ashura ambalo lilijiri takribani miaka 1382 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria Qamaria.

Katika tukio hilo, moja kati ya vita mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu, vilitokea baina ya majeshi ya haki na batili katika ardhi ya Karbala huko Iraq. Siku hii inajulikana kwa jina la Ashura. Katika siku hiyo mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib AS, alisimama kishujaa na wafuasi wake waaminifu 72, kukabiliana na jeshi la batili ili kuilinda dini ya Allah. Hamasa ya Karbala ilikuwa dhihirisho la mambo mawili makuu. Kwanza ni ujasiri, ushujaa, moyo wa kujitolea, uaminifu pamoja na kuyapokea kwa moyo mkunjufu mauti ya kuuawa shahidi, sifa walizojipamba nazo wapiganaji wachache wa jeshi la haki wakiongozwa na Imam Hussein AS dhidi ya Yazid bin Muawiya.

Wimbi la mwamako wa Imam Hussein AS dhidi ya madhalimu lilikuwa na taathira hiyo ilikuwa kubwa mno kiasi kwamba haikuishia kwenye wakati, zama au eneo makhsusi bali imeendelea kufanyakazi yake kati ya wanadamu wote hadi katika zama hizi. Ukweli huu umethibitisha msemo unaosema: "Kila siku ni Ashura na kila ardhi ni Karbala."

3475478/

Kishikizo: ismaili ، muharram ، ashura ، imam hussein as ، karbala