Akizungumza na waandishi habari siku ya jumatano, Katibu MKuu wa Jumuiya hiyo Ayatullah Muhsin Araki alisema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inahimiza Umoja na Mshikamano miongoni mwa Waislamu wote duniani. Alitoa wito kwa vyombo vya habari na wanazuoni katika nchi za Kiislamu kuhubiri umoja na mshikamano ili kuzuia fitna katika Ummah. Ayatullah Araki ameelezia matumaini yake kuwa juhudi za kukurubisha madhehebu ya Kiislamu zitazaa matunda na kuangamiza fitina ya Wazayuni dhidi ya Ulimwengu wa Kiislamu.
Sheikh Araki amesema Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu Tehran utahudhuriwa na takribani maulamaa , wasomi na shakhsia 400 muhimu kutoka nchi mbali mbali za Kiislamu. Ameongeza kuwa kongamano la mwaka huu litajumuisha Wiki ya Umoja wa Kiislamu, Siku ya Kimataifa ya Mtume Mohammad SAW, sherehe za Maulid ya Mtume Mtukufu SAW na pia mkakati kuhimiza Utamaduni wa Mtume SAW.
1331621