IQNA

Makkah: Mradi Mpya wa Lango la Mfalme Salman Kuongeza Maeneo ya Sala katika Msikiti Mkuu wa Makka

7:38 - October 17, 2025
Habari ID: 3481376
IQNA – Katika juhudi za kuboresha huduma kwa mahujaji na wakazi wa Makkah, kampuni ya RUA Al Haram Al Makki imetangaza mradi mkubwa wa maendeleo unaojulikana kama Lango la Mfalme Salman , utakaojengwa karibu na Msikiti Mkuu wa Makkah. Mradi huu utaongoza takriban maeneo 900,000 ya kuswali ndani na nje ya jengo.

Mradi huu utachukua eneo la takriban mita za mraba milioni 12, ukilenga kuboresha uwezo wa waumini kufanya ibada katika Msikiti Mkuu wa Makka kupitia miundombinu ya kisasa na usafiri wa umma. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Saudi (SPA), mradi huu utachangia katika kurahisisha uwezo wa waumini kufika katika Msikiti Mkuu na kuinua ubora wa huduma.

Mbali na maeneo ya ibada, mradi la Lango la Mfalme Salman utajumuisha maeneo ya makazi ya kisasa, huduma za hoteli na biashara, kituo cha utamaduni na urithi, na ukarabati wa takriban mita za mraba 19,000 za maeneo ya kihistoria ili kuhifadhi utambulisho wa kiutamaduni wa Makkah

Mradi huu ni sehemu ya malengo ya kiuchumi chini ya dira ya Saudi Vision 2030, ukitarajiwa kuunda zaidi ya ajira 300,000 kufikia mwaka 2036.

Kwa mujibu wa tangazo la Mwana Mfalme Mohammed bin Salman, mradi wa Lango la Mfalme Salman unalenga kuibadilisha Makkah kuwa mfano wa kimataifa wa maendeleo endelevu ya mijini, huku ikihifadhi urithi wa Kiislamu na kuboresha safari ya kila mgeni wa Msikiti Mtakatifu wa Makka.

3495034

Kishikizo: makka msikiti
captcha