IQNA

Sheikh Ahmed Nuaina Achaguliwa Kuwa Sheikh al-Qurra wa Misri

7:45 - October 17, 2025
Habari ID: 3481377
IQNA-Wizara ya Wakfu wa Kidini ya Misri imemteua rasmi Qari Dkt. Ahmed Ahmed Nuaina kuwa Sheikh al-Qurra, yaani Kiongozi Mkuu wa Wasomaji wa Qur'anI nchini humo.

Utumishi wa Nusu Karne kwa Qur'an

Katika amri rasmi ya uteuzi, Waziri Sheikh Osama al-Azhari alitambua mchango wa Sheikh Nuaina kwa zaidi ya miaka hamsini katika kuhifadhi na kufundisha Qur'ani Tukufu. Sheikh Al-Azhari alimwelezea kama mfano wa ustadi, unyenyekevu na heshima, ambaye amehamasisha vizazi vya wasomaji wa Qur'ani ndani ya Misri na ulimwenguni kote.

Sheikh Nuaina alitoa shukrani zake kwa uteuzi huo, akiomba mafanikio na ikhlasi katika kutekeleza majukumu ya nafasi hiyo tukufu.

Waziri pia alitangaza kuundwa upya kwa Baraza Kuu la Usomaji Qur'ani Tukufu ndani ya wizara, likiwa na lengo la kuendeleza miradi ya Qur'an na kuratibu vyema vituo vya usomaji nchini. Baraza hilo litakuwa chini ya uenyekiti wa waziri na linajumuisha:

  • Qari Dkt. Ahmed Ahmed Nuaina – Sheikh al-Qurra wa Misri
  • Sheikh Abdul Fattah Taruti – Naibu Sheikh al-Qurra
  • Sheikh Mahmoud Muhammad Hassan al-Khesht – Naibu Sheikh al-Qurra

Maisha na Elimu

Sheikh Nuaina alizaliwa mwaka 1954 katika kijiji cha Matubas, mkoa wa Kafr al-Sheikh. Alikamilisha kuhifadhi Qur'an yote akiwa na umri wa miaka minane, kisha akaendelea na masomo ya udaktari katika Chuo Kikuu cha Alexandria, ambako alihudumu katika hospitali mbalimbali.

3495033

 

captcha