
Kwa mujibu wa Al-Kafeel News, mashindano haya yameandaliwa na Idara ya Usimamizi wa Kitaaluma na Tathmini ya Kitengo cha Shughuli za Wanafunzi katika Wizara ya Elimu ya Juu na Utafiti wa Kitaaluma ya Iraq, kwa msaada wa Haram Takatifu ya Hadhrat Abbas (AS). Yalianza tarehe 12 Oktoba na kuendelea hadi 16 Oktoba.
Sherehe ya ufunguzi ilijumuisha usomaji wa Qur'ani kutoka kwa qari wa Iraq, Mohammed Redha al-Zubaidi, hotuba ya Dkt. Maitham Hamid al-Qanbar (Makamu wa Rais wa Masuala ya Kitaaluma wa Chuo Kikuu cha Al-Ameed), mwakilishi wa Wizara ya Elimu ya Juu, na Dkt. Alaa al-Mousawi, Naibu Mkuu wa Bunge la Sayansi ya Qur'an linalohusiana na haram hiyo. Kipindi hicho pia kilipambwa na uimbaji wa tawasheeh na kutambua mchango wa vyuo vikuu vilivyoshiriki.
Jopo la majaji lilihusisha wataalamu wa fani mbalimbali za Qur'ani ambao ni Dkt. Basim al-Abbadi (usomaji na ibtida’) Sheikh Mahdi al-Amiri (uhifadhi) Sheikh Mohammed Fahmi Asfour (kanuni za tajwid) Yahya al-Sahhaf (sauti) Sayyid Hassanayn al-Hulw (melodi)
Mushtaq Karim Abdulrahim, Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu cha Al-Ameed kwa Masuala ya Utawala na Sheria, alisema: "Mashindano haya ni sehemu ya shughuli za Wizara ya Elimu ya Juu na Utafiti wa Kitaaluma. Wanafunzi kutoka nchi za Kiarabu na za kigeni, pamoja na wawakilishi wa vyuo vikuu 60 vya Iraq, walishiriki."
Aliongeza: "Kwa kuzingatia athari yake katika kuinua ari ya wanafunzi kwa kuunganisha Qur'ani Tukufu na mazingira ya chuo kikuu, mashindano haya ni miongoni mwa shughuli muhimu za Qur'ani zinazoungwa mkono na Chuo Kikuu cha Al-Ameed. Haram Takatifu imekuwa ikitekeleza mkakati huu kwa niaba ya vyuo vya Al-Ameed na Al-Kafeel."
Mashindano haya ni sehemu ya mfululizo wa matukio yanayolenga kujenga kizazi chenye fahamu, kilicho na maadili ya kidini na dhamira ya kiroho.
3495032