IQNA

Vyuo Vikuu Bora Vyaenziwa katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ‘Al-Nur’ nchini Iraq

7:58 - October 18, 2025
Habari ID: 3481380
IQNA-Hafla ya kuvienzi vyuo vikuu vilivyofanya vyema pamoja na kamati ya majaji walioshiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya vyuo vikuu, yaliyopewa jina la "Al-Nur", imefanyika katika Chuo Kikuu cha Al-Ameed nchini Iraq.

Mashindano haya yaliandaliwa kwa juhudi za Idara ya Usimamizi na Tathmini ya Kitaaluma ya Wizara ya Elimu ya Juu na Utafiti wa Kitaaluma ya Iraq, kwa msaada wa Idara ya Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Hadhrat Abbas  (AS), kuanzia tarehe 12 hadi 16 Oktoba mwaka huu.

Katika hafla hiyo, vyuo vikuu vinane bora kutoka Iraq na vyuo vikuu vitatu vya kimataifa vilitambuliwa kwa mchango wao wa kipekee na ushiriki wenye athari katika mashindano hayo.

Vilevile, wajumbe wa kamati ya majaji walitunukiwa kwa kutambua juhudi zao katika kufanikisha mashindano hayo na kuhakikisha haki katika tathmini ya washiriki.

Hafla hiyo ilihudhuriwa rasmi na Baraza la Kitaaluma la Qur’ani Tukufu la Idara ya Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Hadhrat Abbas  (AS), uongozi wa Chuo Kikuu cha Al-Ameed, wawakilishi kutoka Wizara ya Elimu ya Juu, vyuo vikuu shiriki, pamoja na baadhi ya wahadhiri na wanafunzi.

Hitimisho la mashindano haya lilijumuisha mtihani kwa wanafunzi wa kimataifa waliokuwa washiriki, na baadaye kutangazwa kwa matokeo ya mwisho ambapo vyuo vikuu vinane vya Iraq na vitatu vya kimataifa vilichaguliwa kuwa bora katika fani mbalimbali.

Mashindano haya yalihitimishwa kwa ugawaji wa tuzo za ubora kwa vyuo vikuu vinane vya Iraq na tuzo za heshima kwa vyuo vikuu vitatu vya kimataifa, kama ishara ya kuthamini mchango wao wa kipekee katika tukio hili adhimu la Qur’ani.

4311210

Habari zinazohusiana
captcha