Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani IQNA, tovuti ya www.egypty.com imeripoti kuwa mtoto huyu kutoka Algeria ana umri wa miaka mitatu na amewavutia watu wengi kote duniani kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuhifadhi aya zote za Qur'ani na kusoma kutoka moyoni. Aidha ana uwezo mzuri wa kusoma Qur'ani kwa mbinu ya tarteel. Imearifiwa kuwa ameihifadhi Qur'ani kwa kushiriki katika vyuo vya Qur'ani na misikitini. Mtoto huyo Mualgeria alianza kuhifadhi Qur'ani akiwa na umri wa miaka miwili wakati alipoanza kuzungumza na alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani yote kwa muda wa mwaka moja. Kanali ya televisheni ya MBC imerusha hewani ripoti kuhusu mtoto huyo mwerevu na kusema Abdu-Rahman ana kipaji cha kipekee cha kusoma Qur'ani kwa tarteel kwa kuzingatia kanuni zote za usomaji pasina kufanya kosa. Mtoto huyo awali kabisa alihifadhi Surah Al Kahf. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mama yake mtoto huyo alikuwa akisoma sana Surah Al Kahf wakati akiwa mja mzito kutokana na kuwa surah hiyo ilikuwa ikimpa utulivu mkubwa wa moyo.
1384655