IQNA

Ali Larijani

Iran inataka udugu na mwamko wa Kiislamu

20:52 - September 09, 2014
Habari ID: 1448576
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani bunge la Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inataka kuimarisha umoja, udugu na mwamko wa Kiislamu katika ulimwengu wa Kiislamu.

Ali Larijani ameyasema hayo leo mjini Tehran alipohutubu katika Kongamano la Kimataifa la 'Maulamaa wa Kiislamu Wanaounga Mkono Harakati ya Muqawama (mapambano) ya Wapalestina.' Larijani amesisitiza kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamewaletea Waislamu umoja na kuongeza kuwa, katika hotuba za Imam Khomeini MA, neno linaloonekana zaidi ni umoja na heshima kwa ajili ya Waislamu.

Larijani ameongeza kuwa lengo kuu la nchi za Magharibi kuunda utawala wa Kizayuni wa Israel ni kuibua mifarakano na kuvuruga umoja wa Waislamu. Kongamano hilo la siku mbili pia limehutubiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu Ayatullah Mohsen Araqi, Ramadhan Abdullah Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina ambaye alihutubu kwa njia ya video na rais wa zamani wa Visiwa vya Comoro Ahmed Abdallah Mohamed Sambi. Katika hotuba yake Sambi ameelezea matumaini kuwa kongamano hilo la Tehran litajadili na kutafutia ufumbuzi changamoto za ulimwengu wa Kiislamu zikiwemo za kisiasa na kiuchumi na hasa kadhia ya Palestina.

 

captcha