IQNA

Ajuza mwenye umri wa miaka 70 ahifadhi Qur'ani nzima Saudia

20:35 - October 14, 2014
Habari ID: 1460246
Ajuza mwenye umri wa miaka 70 amefanikiwa kuhifadhi Qur'ani nzima baada ya juhudi kubwa za miaka 15.

Gazeti la al Wiam limeandika kuwa, ajuza huyo mwenye umri wa miaka 70 amefanikiwa kushika kichwani na kuhifadhi Qur'ani nzima  kutokana na jitihada zake kubwa na irada madhubuti licha ya umri wake mkubwa.
Mkuu wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'ani katika eneo la Afif nchini Saudi Arabia Muhammad al Abdan amesema kuwa kitengo cha wanawake cha jumuiya hiyo kimefanya sherehe maalumu ya kumuenzi ajuza huyo aliyefanikiwa kuhifadhi Qur'ani nzima.
Ameongeza kuwa jumuiya hiyo imemuenzi na kumsifu ajuza huyo mwema kwa kupata fahari hiyo kubwa ya kuhifadhi Qur'ani nzima.   1459360

Kishikizo: Ajuza, Qur'ani, saudia
captcha