IQNA

Mrithi wa Ufalme wa Uingereza asisitizia juu ya kuwepo mazungumzo kati ya dini mbalimbali

16:05 - November 03, 2008
Habari ID: 1704100
Mwanamfalme Charles wa Uingereza amesema katika mazungumzo yake na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislamu ya Muhammadiyyah ya Indonesia kwamba kuna udharura wa kueneza utamaduni wa mazungumzo kati ya wafuasi wa dini za Kiislamu na Kikristo.
Gazeti la Jakarta Post limeandika kuwa Mwanamfalme Charles ambaye yuko katika safari ya siku tano ya kuitembelea Indonesia amesema, hekima na busara ya dini mbalimbali duniani inaweza kusaidia juhudi za kupambana na maadui wa pamoja ikiwa ni pamoja na umaskini na kubakia nyuma kimaendeleo.
Mwanamfalme Charles wa Uingereza anatarajiwa kukutana na Rais Susilo Bambang Yudhoyono wa Indonesia hii leo. Pande hizo mbili zitajadili matatizo yanayowakabili wafuasi wa dini mbalimbali duniani. 314515
captcha