IQNA

Polisi ya Norway kuchunguza hali ya polisi wenye vazi la hijabu

12:12 - November 05, 2008
Habari ID: 1704832
Polisi ya Norway imesema imeazimia kuchunguza hali ya vazi la hijabu la polisi wa nchi hiyo wanapokuwa kazini.
Mwandishi wa kujitolea wa IQNA amesema kuwa, kadhia hiyo ilianza baada ya polisi mmoja mpya Muislamu kuwauliza maafisa wa chuo cha upolisi kwamba je, anaweza kutumia vazi la hijabu kazini au la?
Mkuu wa eneo la Rogaland huko Norway amesema kuwa sura za kidini za wanaume na vazi la hijabu la polisi wa kike vinadhihiri zaidi siku baada ya siku na kwamba idara ya polisi inapaswa kulitilia maanani suala hilo sambamba na mabadiliko hayo ya mavazi katika jamii.
Mkuu wa polisi ya mji mkuu wa Norway, Oslo amesema, analitaza suala la vazi la hijabu la polisi wa kike kwa mtazamo chanya na kuongeza kuwa haja za aina mbalimbali hujitokeza katika vipindi tofauti, suala ambalo amesisitiza kwamba, haliwezi kufumbiwa macho. Kamanda wa polisi ya mji wa Oslo amesema, hapingi suala la watu kusalijiwa katika jeshi la polisi wakiwa na sura na mavazi tofauti na kwamba vazi kama hilo katika jeshi la polisi ni dafina yenye thamani kwao. 315654
captcha