Gazeti la Khalij Times limeandika kuwa lengo la maonyesho hayo yanayowashirikisha wanahakati wa kiuchumi na wawekezaji kutoka vituo vya fedha vya Kiislamu ni kutayarisha uwanja mzuri wa kustawisha bidhaa halali kote duniani.
Katika maonyesho hayo ya siku tatu yanayozishirikisha nchi kadhaa za Kiislamu na zisizokuwa za Kiislamu, kutaonyeshwa baadhi ya vielelezo vya ustawi wa uwekezaji wa Kiislamu. Vilevile vikao vitatu vya kitaalamu kuhusu benki ya Kiislamu vitafanyika kandokando ya maonyesho hayo. 319480