IQNA

Shule ya Qur’an yazinduliwa katika mkoa wa Osh, Kyrgyzstan

22:09 - July 15, 2026
Habari ID: 3482490
IQNA – Shule mpya ya Qur’an imezinduliwa katika eneo la Myrza-Ake, katika mji wa Uzgen, Mkoa wa Osh, nchini Jamhuri ya Kyrgyzstan.

Shule hiyo ya Qur’an imejengwa na Shirika la Ulimwengu la Vijana wa Kiislamu (WAMY). Takriban wakazi 3,800 wa eneo hilo na jamii jirani wanatarajiwa kunufaika na huduma za shule hiyo.

Shule hiyo inalenga kutoa mazingira jumuishi ya kielimu kwa ajili ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu na kusoma sayansi zake. Aidha, inalenga kukidhi mahitaji ya kielimu ya wakazi wa eneo hilo na kuimarisha maadili ya Kiislamu miongoni mwa vijana.

Wakazi wa Myrza-Ake wameeleza shukrani zao za dhati kwa kuanzishwa kwa shule hiyo, wakisema kuwa itakuwa ni alama muhimu ya kielimu yenye athari chanya katika maisha ya watoto wao.

Kyrgyzstan ni nchi isiyo na bandari, yenye mandhari ya milima katika eneo la Asia ya Kati. Imepakana na Kazakhstan kwa upande wa kaskazini, Uzbekistan kwa upande wa magharibi na kusini-magharibi, Tajikistan kwa upande wa kusini-magharibi, na China kwa upande wa mashariki. Mji wake mkuu na mkubwa zaidi ni Bishkek.

Vyanzo rasmi vinakadiria kuwa asilimia 80 ya wakazi wa nchi hiyo ni Waislamu.

/3498267

captcha