Washiriki watashindana katika nyanja mbalimbali za kuhifadhi (hifdhi), usomaji (tajwid), na tafsiri ya Qur’ani Tukufu. Mashindano haya ya mwaka huu yatafanyika chini ya usimamizi wa Wizara ya Awqaf na Mambo ya Kiislamu ya Morocco, kwa mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW).
Kwa mujibu wa tangazo la Wizara ya Awqaf ya Morocco, kundi la mahafidh na wasomaji wa Qur’ani kutoka nchi za Kiarabu, Kiislamu, Afrika, Asia, Ulaya, na Amerika watakuwepo katika tukio hili adhimu la Qur’ani.
Sherehe za ufunguzi wa mashindano haya ya kimataifa zimepangwa kufanyika Jumatatu, tarehe 19 Agosti, saa 10:30 asubuhi kwa saa za huko.
Taasisi ya Mohammed VI ya Mafunzo na Elimu kwa Maimamu, Wahubiri, na Wanaharakati wa Kiislamu (Missionaries) jijini Rabat ndiyo itakayokuwa mwenyeji wa hafla hiyo.
4363192