Basem Naim, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, ametoa pongezi kwa timu ya taifa ya Uhispania kwa “ushindi wake wa haki.”
Pia ametuma salamu za pongezi kwa watu wa Palestina na wafuasi wao kote ulimwenguni ambao walisherehekea ushindi huo kwa shauku kubwa.
Naim amesema: “Kama ushindi huu haukuwa na mafanikio mengine isipokuwa kuwakera Wazayuni na mamluki wao, hiyo ingekuwa inatosha.”
Ushindi wa Uhispania umewafurahisha watu kote Palestina na miongoni mwa wafuasi wa mhimili wa Muqawama ulimwenguni kote. Timu ya Uhispania imekuwa ishara ya mshikamano na kadhia ya Palestina, kwa sehemu kubwa kutokana na msimamo wa kisiasa wa kikanuni wa Uhispania dhidi ya mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala wa Israel huko Gaza.
Aidha, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel alitangaza wazi kuunga mkono timu ya Argentina kutokana na ukweli kwamba nyota wa timu hiyo, Lionel Messi, ni mfuasi mkubwa wa Wazayuni. Nukta hii pekee imewafanya wengi duniani kuinga mkono Uhispania.
Serikali ya eneo la Madrid nchini Uhispania imetambua Taifa la Palestina, imeweka vikwazo dhidi ya utawala huo vamizi, na kuvunja uhusiano wa kidiplomasia ikiwa ni jibu kwa mauaji na uharibifu unaofanywa dhidi ya watu wa Palestina.
Aidha, nyota wa Uhispania Lamine Yamal, ambaye amekuwa shujaa huko Gaza, aliwahi kupeperusha bendera ya Palestina wakati wa sherehe za ubingwa wa La Liga wa Barcelona, kitendo ambacho kilichochea kuchorwa kwa michoro ya mchezaji huyo kijana katika vitongoji vilivyoharibiwa na vita katika eneo hilo lililozingirwa na Israel.
Aidha, msimamo wa Uhispania wa kupinga vita vya kigaidi vya Marekani na Israel dhidi ya Iran umewavutia wengi duniani kote ambao wameishabikia timu hiyo.
Ushindi wa Uhispania, ingawa ni mafanikio ya michezo, unabeba uzito mkubwa wa kisiasa kwa kuangazia kutengwa kwa utawala wa Kizayuni katika jukwaa la kimataifa na kuchukizwa kwa jamii ya kimataifa na uhalifu wake.
Wakati watu wa Palestina wakiendeleza mapambano yao ya kishujaa, matukio kama haya hutumika kama ukumbusho kwamba kadhia ya haki inavuka mipaka. Furaha iliyopo Palestina na miongoni mwa wafuasi wake kufuatia mafanikio ya Uhispania inasisitiza roho isiyoweza kuvunjika ya taifa linalokataa kufutika, hata linapokabiliwa na mojawapo ya mashambulizi ya kikatili zaidi katika historia ya kisasa.
Uhispania imeibuka bingwa wa Kombe la Dunia baada ya kuichapa Argentina bao 1-0 katika fainali iliyohitaji muda wa nyongeza, huku Ferran Torres akifunga bao la ushindi lililowavunja nguvu mabingwa watetezi. Fainali hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa MetLife, New Jersey, ilimalizika bila mabao ndani ya dakika 90 za kawaida na hivyo kuamuliwa katika muda wa nyongeza.
Fainali hiyo ilikuwa ya ushindani mkubwa, ikipewa uzito zaidi na mapambano ya kimwili na tahadhari za pande zote kuliko soka la kushambulia. Hata hivyo, nje ya uwanja kulikuwa na shamrashamra kubwa, huku mastaa mbalimbali wakihudhuria kushuhudia mechi hiyo ya kihistoria.
3498338