IQNA

Vijana 600 waliohifadhi Qur’ani Tukufu waenziwa Ukanda wa Gaza

16:33 - July 24, 2026
Habari ID: 3482530
gaza
IQNA – Hafla maalumu imeandaliwa kwa ajili ya kuwatunuku zawadi na kuwaenzi vijana 600 waliohifadhi Qur’ani Tukufu katika Ukanda wa Gaza.

Hafla hiyo imeandaliwa na operesheni ya Chivalrous Knight 3 kwa kutambua juhudi za watoto hao katika kuhifadhi Qur’ani Tukufu na kuwahamasisha waendelee na safari yao ya kielimu na kidini.

Tukio hilo ni sehemu ya programu za kibinadamu na kijamii za operesheni hiyo, zinazolenga kuwasaidia watoto na kuendeleza maadili mema katika mazingira ya kipekee yanayoukabili Ukanda wa Gaza.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na maelfu ya wanafamilia pamoja na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za Qur’ani na kijamii, zikiwemo Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini, Jumuiya ya Iqraa, Dar Al-Quran Al-Kareem, Dar Al-Itqan, Jumuiya ya Vijana Wanawake Waislamu, Chuo cha Al-Safa na Jumuiya ya Al-Sahaba.

Ratiba ya hafla hiyo ilijumuisha visomo vya Qur’ani, qasida na madih ya kidini, pamoja na kuwatambua watoto waliofanya vyema na wahifadhi bora wa Qur’ani, katika mazingira ya fahari na shangwe yaliyoakisi azma ya watoto hao na mshikamano wao kwa maadili yao.

Hafla hiyo ilihitimishwa kwa utoaji wa zawadi na misaada ya kifedha kwa watoto waliotunukiwa, kwa lengo la kuwaletea furaha na kuwatia moyo waendelee kuhifadhi Qur’ani Tukufu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za operesheni ya Chivalrous Knight 3 za kuunga mkono mipango inayokuza matumaini na kuwatunza vizazi vya vijana katika Ukanda wa Gaza.

Pamoja na kuwa Ukanda wa Gaza unakabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala haramu wa Israel, lakini Wapalestina katika eneo hilo wameendelea kushikamana na shughuli za Qur'ani Tukufu bila kusita jambo linaloashiria imani yao thabiti ambayo ni mfano wa kuigwa duniani kote.

Ikumbukwe kuwa Utawala wa Kizayuni wa Israel ulianzisha mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Gaza mnamo Oktoba 7 mwaka 2023 kabla ya usitishwaji vita Oktoba mwaka jana. Katika kipindi hicho cha mauaji ya kimbari, Israel iliwaua Wapalestina wasipungua 73,000, wengi wakiwa ni wanawake na Watoto. Aidha utawala wa Isarel umeharibu karibu asilimi 90 ya maeneo yote ya makazi ya watu wa Gaza na kulifanya eneo hilo kuwa magofu. Waziri Mkuu wa utawala katili wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wake wa zamani wa vita Yoav Gallan wanasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kutokana na jinai walizotenda huko Gaza.

Nchi kadhaa zimetangaza kuwa tayari kumakamata Netanyahu na kumkabidhi kwa mahakama hiyo ya kimataifa iwapo atakanyaga ardhi zao.Majaji wa ICC walitoa kibali cha kukamatwa Netanyahu na Gallant Novemba mwaka 2024. Aidha Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) imeitaka Israel isitishe sera za mauaji ya kimbari huko Gaza. Watawala wa Israel wamepuuza taasisi hizo za kimataifa na wanaendeleza jinai zao dhidi ya Wapalestina.

3498391

Habari zinazohusiana
captcha