Kituo cha Mfalme Fahd cha Uchapishaji wa Qur’ani Tukufu ya Saudi Arabia kimeweka tarjuma hizo Qur’ani Tukufu kupitia tovuti yake rasmi.
Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi zake zinazoendelea za kutumia teknolojia ya kisasa kwa ajili ya kuitumikia Qur’ani Tukufu na kupanua fursa ya walimwengu kufikia maana zake.
Tarjuma hizo zinapatikana katika wigo mpana wa lugha za Asia, Ulaya na Afrika, na zimeandaliwa pamoja na kuhakikiwa kwa mujibu wa utaratibu madhubuti wa kielimu chini ya uangalizi wa jopo la wataalamu, ili kuhakikisha usahihi na uaminifu wa maana zilizotafsiriwa.
Mpango huo unawawezesha wasiokuwa wazungumzaji wa Kiarabu kufahamu Qur’ani Tukufu kupitia jukwaa la kisasa la kidijitali lililo rahisi kulitumia.
Taasisi hiyo imeeleza kuwa tarjuma zote zinapatikana bure kwa kupakuliwa na kutumiwa kupitia tovuti yake, jambo linalosaidia kueneza kwa upana zaidi maana za Qur’ani Tukufu na kuimarisha uwepo wake wa kidijitali katika ngazi ya kimataifa.
3498380