IQNA

15:23 - July 22, 2026
Habari ID: 3482526

Ziara tukufu ya Arbaeen itafanyika kwa usalama wa hali ya Juu

TEHRAN – Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa hatua zote muhimu zimechukuliwa ili kuhakikisha kuwa ziara ya Arbaeen inafanyika kwa utaratibu, usalama, na utulivu wa hali ya juu.

 Ali Zeinivand

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Ali Zeinivand alibainisha kuwa wizara hiyo imejipanga kikamilifu katika nyanja za kiusalama, kisheria, na utoaji wa huduma kwa ajili ya mamilioni ya mazuwar watakaoshiriki katika safari hii tukufu. Alisisitiza kuwa “Makao Makuu ya Arbaeen” yamekuwa yakifanya mikutano ya mara kwa mara ili kufuatilia na kutatua changamoto zozote zinazoweza kujitokeza.

Zeinivand alikumbusha uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kusimamia mikusanyiko mikubwa ya kidini, akitolea mfano wa jinsi ibada ya Arbaeen ilivyofanyika kwa mafanikio makubwa mwaka uliopita. Aidha, aliongeza kuwa hafla za mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu zilihudhuriwa na umati mkubwa sawa na au zaidi ya ule wa Arbaeen, tukio ambalo lilifanyika kwa usalama wa kipekee na bila kasoro yoyote; jambo linalothibitisha uthabiti wa mfumo wa usalama wa nchi hiyo.

Kuhusu maandalizi ya mipakani, msemaji huyo alibainisha kuwa mkuu wa Makao Makuu ya Arbaeen amefanya ziara za kukagua vituo vikuu vya mpaka, ikiwemo Chazabeh, Shalamcheh, Mehran, Somar, na Khosravi. “Kwa bahati nzuri, hakuna changamoto zozote za kimsingi katika vituo hivi, na vikosi vya ulinzi na usalama viko imara mipakani ili kuhakikisha usalama, ustawi, na urahisi wa usafiri kwa mazuwar,” alisisitiza Zeinivand.

Mbali na raia wa Iran, Iran imeweka mazingira wezeshi kwa mazuwari kutoka nchi jirani na mbali zaidi, ikiwemo Afghanistan, Pakistan, nchi za Asia ya Kati, Caucasus, na Uturuki, wanaotaka kushiriki katika safari hii ya kuelekea Karbala.

Arbaeen ni maadhimisho matukufu ya kidini yanayofanywa na Waislamu, hususan wa madhehebu ya Shia, katika siku ya arubaini baada ya Siku ya Ashura, kuadhimisha kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na Imam wa tatu wa Waislamu wa madhehebu a Shia.

Hii ni moja ya ziyara kubwa zaidi za kila mwaka ulimwenguni, ambapo mamilioni ya Waislamu wa Shia, pamoja na idadi kubwa ya Masunni na wafuasi wa dini nyinginezo, hutembea kwa miguu kuelekea mji mtukufu wa Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani. Mwaka huu, siku ya Arbaeen inasadifia tarehe 4 Agosti.

Safari hii inasalia kuwa mojawapo ya ziyara kubwa zaidi ya kidini duniani, ikijumuisha mamilioni ya waumini wanaotembea kwa miguu kuelekea Karbala, Iraq, wakionyesha umoja na mapenzi yao kwa njia ya haki na uadilifu. Mwaka huu, siku ya Arbaeen inatarajiwa.

3498373

Habari zinazohusiana
captcha